IQNA

'Siku ya Wazi' msikitini Texas Marekani kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu

17:02 - February 02, 2022
Habari ID: 3474882
TEHRAN (IQNA) – Msikiti mmoja huko Texas Marekani unapanga 'Siku ya Wazi' ya kuwakaribisha wasiokuwa Waislamu ili kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia).

Kwa mujibu wa taarifa, Kituo cha Kiislamu Texas kimepanga kufungua milango ya msikiti huo kwa wasiokuwa Waislamu Jumamosi 5 kuanzia saa tano hadi saa nane mchana.

Wanaoandaa tukio hilo wanasema wanalenga kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu kwa kuwakaribisha majirani msikitini ili waweze kufahamu Uislamu.

Tukio hilo limeandaliwa na taasisi za Kiislamu ambazo ni WhyIslam, GainPeace na Jumuiya ya Kiislamu ya Texas Kaskazini.

"Sisi kama Waislamu tunafungua milango ya misikiti yetu ili kuwezesha jamii kuwaelewa Waislamu, amesema Sabeel Ahmed, mkurugenzi wa GainPeace.

/3477647

captcha