IQNA

Maadili ya Uislamu

Qatar kuonyesha Hadithi za Mtume Muhammad SAW wakati wa Kombe la Dunia

7:23 - November 01, 2022
Habari ID: 3476017
TEHRAN (IQNA) - Qatar imetayarisha maandishi makubwa ya hadithi za Mtume Muhammad (SAW) yatakayowekwa maeneo muhimu wakati wa Kombe la Soka la Dunia la 2022.

Katika kujiandaa na Kombe la Dunia linalotarajiwa kwa hamu, Qatar imepanga kuonyesha utamaduni na maadili yake ya Kiislamu kwa  wageni watakaofika nchini humo kwa ajili ya Kombe la Dunia. Moja ya mbinu ambazo Qatar inatumia  ni kuweka maonyesho ya Hadithi za Mtume Muhammad (SAW) kote katika nchi hiiyo ili kutambulisha Uislamu kwa watakaoshiriki katika Kombe la Dunia.

Maneno hayo yalioezekwa katika maeneo muhimu yana maneneo mbalimbali ya Mtume Muhammad SAW kuhusu rehema, hisani na matendo mema.

"Kila tendo jema ni sadaka", "Asiyekuwa na huruma kwa wengine, hatatendewa huruma", na "Jilinde na Moto wa Jahannamu, hata kwa nusu ya tende katika sadaka. Ikiwa mtu hawezi kuipata, basi atamke neno la ukarimui" ni baadhi ya Hadith za Mtume SAW zinazoonekana katika mitaa mbali mbali ya Qatar.

Kombe la Dunia la FIFA 2022 nchini Qatar limeratibiwa kuanza Novemba 20 hadi Desemba 18.

Mashindano ya mwaka huu ni ya kwanza kuandaliwa Mashariki ya Kati au Asia Magharibi, ya kwanza katika nchi yenye Waislamu wengi, na ya kwanza kufanyika mwishoni mwa mwaka, mwezi Novemba na Desemba.

3481064

captcha