IQNA

Sira ya Mtume Muhammad

Mtume Muhammad SAW hakuanzisha vita vyovyote

22:20 - November 05, 2022
Habari ID: 3476040
TEHRAN (IQNA) - Mapitio ya vitabu vya historia yanaonyesha kuwa vita vyote wakati wa Mtume Mtukufu Muhammad (SAW) vilikuwa vya kujihami au kujitetea na kwamba hakuanzisha vita yoyote.

Uchunguzi wa kina wa vitabu kuhusu matukio ambayo yalifanyika katika enzi ya Mjumbe wa Mwisho wa Mungu unaonyesha kwamba mwenendo wa Mtukufu Mtume Muhammad (PBUH) na njia aliyotumia ya kushughulikia maswala tofauti ulikuwa wa kipekee.

Kulingana na vyanzo vya kihistoria, vita kuu nne au vitano vilijiri katika enzi hiyo. Wanahistoria wanasema kwamba vita hivi vyote dhifi Kuffar (makafiri) vilikuwa vya kujijami na kwamba Mtume (PBUH) aliwaambia Masahaba zake wasianzishe vita yoyote kabla ya adui kufanya hivyo.

Wakati wa Imam Ali (AS) (kama mtawala) kulikuwa na vita vitatu na yeye au jeshi lake hawakuanzisha vita.

Njia ya Uisilamu ni ile ya busara na hekima na kwa kuzingatia mafundisho ya dini hii, hakuna mtu anayepaswa kulazimishwa kuwa Muislamu. Aya nyingi za Qur’ani Tukufu zinaashiria ukweli kwamba Uislamu unapendelea amani na uvumilivu kwa dhati.

Kulingana na tafiti, katika aya 100 za Qur’ani Tukufu, zinabainisha wazi kupinga  vita na vurugu.

Kuna msisitizo mkubwa juu ya kuishi kwa maelewano na amani katika aya za Qur’ani na Sira ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Kwa hivyo mtu anaweza kusema kuwa kuibua madai na tuhuma kuwa eti Uislamu kama 'dini ya vurugu' ni jambo lisilo na msingi wala mashiko yoyote.

Ukweli ni kwamba Uislamu sawa na dini zilizotangulia za Mwenyezi Mungu zina asili ya maadili  bora na kwa hivyo hauna uwezekano wa kuhimiza maovu kama vile vita na umwagaji damu.

Imam Ali (AS) alimwandikia barua Malik al-Ashtar, gavana wake wa Misri,  kwamba ili aepuke kabisa kumwaga damu kwa sababu hakuna kitu kinachopelekea kuanguka kwa serikali kama damu ambayo imemwagika bila haki.

Kwa hivyo sababu zilizotajwa kuonyesha Uislamu kama dini ya vita vurugu sio kweli. Badala yake, ukweli kwamba vita vyote vya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) dhidi ya makafiri vilikuwa vita vya kujihami na kujitetea na kwamba Uislamu umewasilisha mikakati mingi ya amani ni sababu kamili za kudhibitisha kuwa Uislamu ni dini ya amani.

Kulingana na vitabu vya historia na vitabu vingine, vitendo vya dhuluma vilivyofanywa kwa jina la Uislamu na Qur’ani vilianza baada ya kufariki kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na kuendelea hadi leo kwa njia ya vikundi vilivyopotoka na vinavyotumiwa na maadui wa Uislamu.

captcha