IQNA

Maafisa wa uhamiaji wafanya upekuzi Msikitini Uingereza

19:11 - November 06, 2022
Habari ID: 3476045
TEHRAN (IQNA) – Maafisa wa uhamiaji wa Uingereza wameongeza upekuzi katika vituo vya kidini, hasa misikitini, katika jitihada za kukabiliana na uhamiaji haramu.

Kama sehemu ya mkakati wa "mazingira ya uhasama", uliozinduliwa mwaka wa 2012 chini ya waziri wa zamani wa mambo ya ndani Theresa May, idara ya uhamiaji imeongeza  mara nne oparesheni za  kutembelea misikiti, mahekalu na makanisa tangu 2019 kwa lengo la kuwasaka  wahamiaji haramu.

Taarifa zinasema mkakati huo ulizinduliwa ili kufanya kukaa nchini Uingereza kinyume cha sheria kuwa vigumu iwezekanavyo, huku serikali ikiwahimiza watu kuondoka nchini humo kwa hiari.

Katika angalau kesi tatu mwaka huu, Idara ya Uhamiaji iliwaelekeza watu moja kwa moja kutoka maeneo ya  kidini hadi viwanja vya ndege na kuwapandisha kwa lazima ndege zinazoondoka nchini.

Idara hiyo ilifanya ziara zaidi ya 400 katika vituo vya kidini katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ikiwalenga wahamiaji haramu na walioshindwa kupata hifadhi.

Shakila Taranum Maan, wa shirika la kuwasaidia wanaokumbwa na unyanyasaji wa nyumbani, Southall Black Sisters, alisema: "Wateja wetu wengi wanadanganywa na kuarifiwa vibaya kuhusu oparesheni hizi."

"Tumezungumza na watu ambao walidhani walikuwa wakienda kupata msaada, lakini badala yake wanashauriwa ni bora kuondoka Uingereza na wanaambiwa, 'hizi ndizo fedha utakazopata.'

"Maafisa wa Ofisi ya Mambo ya Ndani hawajitambulishi vya kutosha, kwa hivyo watu wanatoa habari zao zote za kibinafsi, bila kujua ni nani wanampa maelezo haya.

3481147

Kishikizo: uingereza misikiti
captcha