IQNA

Harakati za Qur'ani Tukufu

Mashindano ya 63 ya Qur'ani Tukufu ya Malaysia yataanza Jumamosi

17:26 - August 16, 2023
Habari ID: 3477445
KUALA LUMPUR (IQNA) – Raundi ya mwisho ya toleo la 63 la mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Malaysia itaanza wikendi hii.

Hafla ya uzinduzi wa hafla hii ya kimataifa ya Qur'ani itafanyika Jumamosi, Agosti 19. Shindano hilo litaendelea kwa wiki moja, huku kukiwa na sherehe za kufunga, ambapo washindi watatangazwa na kutunukiwa, ikipangwa kufanyika Agosti 26. Kama toleo la awali, shindano la mwaka huu lina hatua mbili, huku hatua ya awali ikiwa imefanyika karibu mwezi Juni. Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia, yanayojulikana rasmi kama Mkutano wa Kimataifa wa Kuhifadhi na Kusoma Qur'ani Tukufu wa Malaysia (MTHQA), huandaliwa kila mwaka katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Kuala Lumpur.
Mwaka huu, Ali Reza Bijani atawakilisha Iran katika toleo la 63 la shindano hilo. Aliondoka Tehran kuelekea Kuala Lumpur mapema Jumatano. Amin Pouya anaandamana na Bijani katika safari hiyo kama mwongozaji. Pouya alikuwa ameshika nafasya pili katika toleo la 53 la shindano hilo mnamo 2012. Iran ndiyo yenye idadi kubwa zaidi ya washindi katika hafla hiyo adhimu ya Qur'ani.

Mohammat Taqi Morovat, Abbas Salimi, Ali na Masoud Sayyah Gorgi, Abbas Emamjome, Mansour Qasrizadeh, Ahmad Abolqassemi, Mohsen Hajihassani Kargar na Hamed Alizadeh ni miongoni mwa wasomaji wa Qur'ani wa Iran waliotangulia katika matoleo tofauti ya shindano hilo.
 
4162679

Habari zinazohusiana
captcha