IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Mkanada aliyeua familia ya Kiislamu alichochewa na fikra za wazungu wabaguzi

21:56 - September 12, 2023
Habari ID: 3477589
TEHRAN (IQNA)- Mwanamume mmoja wa Kanada aliyekuwa na msukumo wa fikra za misimamo mikali za kibaguzi za kizungu alitumia gari lake la mizigo kulenga kwa makusudi familiaya Kiislamu kwa na kusababisha vifo vya watu wanne.

Mwendesha mashtaka wa Kanada Sarah Shaikh alisema katika taarifa ya ufunguzi kwamba Nathaniel Veltman, 22, alipanga shambulio hilo kwa muda wa miezi mitatu kabla ya kuendesha gari lake la mizigo aina ya Dodge Ram moja kwa moja kwenye familia ya Waislamu waliokuwa wakitembea kando ya barabara.
Vizazi vitatu vya familia ya Afzaal viliuawa katika shambulio hilo: "Salman Afzaal, 46, mkewe Madiha Salman, 44 binti yao Yumna aliye kuwa na umri wa miaka 15, na Talat Afzaal, nyanyake aliyekuwa na umri wa miaka 74."

Mwana wa wanandoa hao mwenye umri wa miaka tisa pia alijeruhiwa vibaya lakini alinusurika. Alifichua kuwa msukumo wake ulitokana na ufyatulianaji risasi wa 2019 Christchurch, New Zealand ambapo mzungu mwenye misimamo mikali ya kibaguzi aliwaua Waislamu 51 waliokuwa katika Sala ya Ijumaa.
Gaidi hiyo mzungu mwenye misimamo ya kibaguzi anasemekana kuwaambia wapelelezi kwamba: “Sijutii nilichofanya. Nakiri kwamba ulikuwa ugaidi. Hili lilichochewa kisiasa kwa asilimia 100.” 
Kwa mujibu wa taarifa ya Sheikh, alipokamatwa, aliwaambia polisi anataka "kutuma ujumbe mkali" wa kupinga uhamiaji wa Waislamu.
Aliongeza kuwa Veltman alisikika akiwaambia polisi kwa njia ya simu kwamba: "Ni mimi niliyewagonga ... nilifanya makusudi."
Ushahidi uliokusanywa na polisi ulijumuisha maandishi yaliyojaa sifa za itikadi kali za kibaguzi za wazungu dhidi ya uhamiaji, visu kadhaa na bunduki ndani ya gari lake la mizigo.
Veltman amekana mashtaka manne ya mauaji na shtaka moja la kujaribu kuua kuhusu kifo cha familia ya Afzaal jioni ya Juni 2021 huko London, Ontario.
Tukio la kifo cha familia ya Afzaal linasimama kama shambulio mbaya zaidi dhidi ya Uislamu nchini Kanada tangu shambulio la 2017 la msikiti jijini Quebec, ambalo lilisababisha vifo vya watu sita.

Mtu aliyehusika na ufyatuaji risasi wa 2017 hakufunguliwa mashtaka ya ugaidi. Kesi hiyo, ikifuatiliwa kwa karibu, inaweza kurekebisha jinsi Kanada inavyoshtaki itikadi kali za mrengo wa kulia. Kesi hiyo inaashiria mabishano ya mara ya kwanza ya nia ya ugaidi kuhusiana na ukuu wa wazungu ambayo itasikizwa katika mahakama ya Kanada.

Habari zinazohusiana
captcha