IQNA

Jinai za Israel

Askari wa Israel washambulia Wapalestina wakisherehekea Maulid ya Mtume Mohammad (SAW)

10:35 - September 28, 2023
Habari ID: 3477664
AL-QUDS (IQNA) - Vikosi vya utawala katili wa Israel siku ya Jumatano viliwashambulia Wapalestina, wakiwemo wanawake na watoto, ambao walikuwa wakiadhimisha siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) huko Al Quds (Jerusalem) Mashariki. Mji huo mtakatifu unakaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Duru za ndani zilisema vikosi vilimpiga na kumzuilia mtoto wa umri wa miaka 8 na kuwapiga teke wanawake na wasichana kwenye Lango la Damascus, moja ya lango kuu la Mji Mkongwe wa Al Qudsambapo walikuwa wakisherehekea siku ya kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad.

Polisi wa Israel pia hawakuwaruhusu maskauti na bendi za Palestina kufanya gwaride maalumu katika mitaa ya mji kwa mnasaba wa Maulid ya Mtume Muhammad (SAW).

Ikumbukwe kuwa, siku kama ya leo miaka 1498 inayosadifiana na tarehe 12 Mfunguo Sita Rabiul Awwal miaka 53 kabla ya Hijria, kwa kauli ya baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu akiwemo Masoudi, alizaliwa Mtume Muhammad SAW.

Wanachuoni wengine wa Kiislamu wanaamini kwamba, Mtume Muhammad (saw) alizaliwa tarehe 17 Rabiul Awwal mwaka huohuo. Kwa msingi huo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitangaza kipindi cha kuanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul Awwal kila mwaka kuwa ni Wiki ya Umoja kati ya Waislamu kote duniani.

Wiki ya umoja ni fursa nzuri ya kuzikurubisha nyoyo za Waislamu na kuimarisha umoja na mshikamano wao katika kukabiliana na maadui wa ulimwengu wa Kiislamu. 

3485343

captcha