IQNA

Hija katika Uislamu/5

Usahali ni miongoni mwa Sifa Kuu za Hija

18:25 - November 19, 2023
Habari ID: 3477912
TEHRAN (IQNA) – Lengo kuu katika Hija lazima liwe kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na katika safari hii, kadiri tunavyojiepusha na mapambano, kujifaragua na anasa, ndivyo tutakavyokaribia ukamilifu.

Mwenyezi Mungu angeweza kuchagua mawe ya thamani ya kidunia kwa ajili ya ujenzi wa Ka’aba lakini hakufanya hivyo, kwa sababu kadiri itakavyokuwa sahali na isiyo ghali, ndivyo ikhlasi na usafi kutakuwapo. Ka’aba ni bendera ya Uislamu. Bendera ni kipande tu cha nguo lakini jeshi zima linajivunia na maisha mengi yanatolewa kwa ajili yake.

Makka ni mahali ambapo kulala  hapo ni sawa na kujitahidi sana katika maeneo mengine. Kusujudu ndani yake ni kama kufikia kifo cha kishahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Sifa zake haziwezi kueleweka kwa urahisi. Hivyo itakuwa ni jambo la kusikitisha iwapo mahujaji watashindwa kutumia vyema safari hii ya kiroho.

Makka inaitwa Umm al-Qura, ikimaanisha mama wa mikoa. Ni mahali pa wahyi na amani. Kama vile mama anavyowalisha watoto wake, Makka inapaswa kueneza usalama na Risala ya Mitume Muhammad SAW kwa ulimwengu wote.

Mkusanyiko wa watu wanaomwabudu Mwenyezi Mungu katika mji wa Makka, ambao ni mahali ambapo masanamu yalivunjwa, unatupa somo la kuvunja masanamu. Watu kama Abu Dharr na Imam Hussein (AS) walipaza sauti za ujumbe wao karibu na Ka’aba na Imam Zaman (Mwenyezi Mungu aharakishe ujio wake wenye furaha) pia ataanza mwamko wake kutoka hapo.

Yaliyomo katika Hija kwa ujumla na Tawaf (kuizunguka Ka’aba) ni:

Usahali na sio urasimu

Harakati na sio kuganda

Kukumbuka na sio kupuuza

Kufuata amri za Mwenyezi Mungu na kutofuata Mashariki au Magharibi

Mazingira salama sio ufisadi na utovu wa maadili

Rehema na ukarimu sio ubahili,

Kuacha Haramu (iliyoharamishwa) na kutotenda dhambi

Unyenyekevu na upole sio majivuno na kiburi,

Udugu na usawa si ubaguzi na kutafuta ukiritimba.

Hija  ni safari muhimu na yenye kujenga zaidi maishani. Tunapaswa kumwomba Mwenyezi Mungu atupe fursa ya kufaidika na baraka za safari hii. Je, kuna baraka gani kubwa zaidi ya kuwa mgeni wa Mwenyezi Mungu, Mtukufu Mtume (SAW) na Maimamu Maasumin (AS) na kusamehewa dhambi zetu zote.

Ni baraka gani kubwa kuliko kuwa sehemu ya mkusanyiko wa mamilioni ya watu katika sehemu iliyo salama, kuswali, kupiga nara, kujibari au kutangaza kujitenga na washirikina (Bar'aat min-al-mushrikeen), na kutembelea sehemu ambazo matukio muhimu ya historia ya Uislamu yalifanyika. mahali?

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe baraka za kuhiji na kuzuru Ka’aba Tukufu.

Kishikizo: hija
captcha