IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Wawakilishi wa nchi 64 katika mpango wa Kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini Misri

17:53 - December 24, 2023
Habari ID: 3478084
IQNA - Wizara ya Wakfu ya Misri inapanga kuandaa Khatm Qur'an (kusoma Qur'ani Tukufu kuanzia mwanzo hadi mwisho) wiki ijayo.

Harakati hiyo itafanyika kando ya mashindano ya 30 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Misri, yakishirikisha wawakilishi kutoka nchi 64.

Washiriki watasoma Quran kwa mtindo wa Warsh kwa mujibu wa riyawa ya Nafi.

Maqari wakuu wa Misri waliopangwa kushiriki katika hafla hiyo ya Khatm Quran ni pamoja na Ahmed Ahmed Nuaina, Taha Numani, Ahmed Tamim al-Maraghi, Mohamed Fathallah Bibris, Yusuf Qassim Halawah, Fathi Khalif, na Mahmoud Ali Hassan.

Hii ni programu ya tatu ya Qur'ani ya Khatm ya aina hii iliyoandaliwa nchini Misri mwaka huu.

Makala ya 30 ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Misri yataanza Jumamosi, Disemba 23.

Kituo cha Dar-ul-Quran cha Masjid Misri katika mji mkuu mpya wa utawala wa Misri ndicho kitakuwa mwenyeji wa hafla hiyo.  4189390

Habari zinazohusiana
captcha