IQNA

Elimu

Al Azhar yachapisha vitabu vipya vya mafunzo ya Qur'ani Tukufu

18:43 - January 13, 2024
Habari ID: 3478190
IQNA - Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu chenye mafungamano na Chuo Kikuu cha Al-Azhar cha Misri kimechapisha mfululizo wa vitabu vipya vya mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa kituo hicho, vitabu hivyo viko katika fani ya Tafsir (Tafsiri ya Qur'ani) na sayansi nyinginezo za Qur'ani.

Vitabu hivyo vitawasilishwa katika toleo la 55 la Maonesho ya Vitabu ya Kimataifa ya Cairo, ilisema, tovuti ya Akhbar al-Yawm iliripoti.

Dakta Nazir Ayad, mkuu wa Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu cha Al-Azhar, alisema kazi kubwa iliyochapishwa na kituo hicho hivi karibuni ni tafsiri ya juzuu kumi za Qur'ani yenye jina la "Tafsiri ya Wastani ya Qur'ani."

Alisema kitabu hicho kilichotungwa kwa pendekezo la kongamano la nne lililoandaliwa na Akademia ya Masomo ya Kiislamu  inalenga kuwasilisha tafsiri fupi na rahisi kueleweka ya aya za Qur'ani Tukufu

Katika tafsiri hii, mkazo umekuwa kwenye lengo kuu la Qur'an Tukufu, yaani mwongozo, alisema.

Baadhi ya wakosoaji wanasema msisitizo wa kile kinachoitwa "mtazamo wa wastani" katika tafsiri ya Qur'ani unaendana na sera mpya za serikali ya Misri zenye lengo la kuweka vikwazo kwa shughuli za taasisi za kidini.

Wanasema kuwa na  uhusiano wa kiutamaduni na kijamii na utawala wa Kizayuni wa Israel pia ni sehemu ya malengo ya sera mpya za Cairo.

4193465

captcha