IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Iraq: Vipaji vya Qur’ani katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya Al-Ameed

17:44 - April 01, 2024
Habari ID: 3478612
IQNA – Haram Tukufu ya Hadhrat Abbas (AS) huko Karbala hivi karibuni ilihitimisha awamu ya kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani yajulikanayo kama Tuzo ya Kimataifa ya Al-Ameed ya Kusoma Qur’ani, ambayo yamefanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hafla hiyo, iliyoandaliwa na jumba la kisayansi la Qur'ani Tukufu kwenye haram hiyo, lilishuhudia ushiriki wa maqari kutoka nchi 21.

Mashindano hayo ya Qur'ani yalifanyika kwa zaidi ya vipindi kumi vya kusisimua, huku washiriki wakichuana kusonga mbele katika duru hizo. Baada ya duru kadhaa za ushindani mkali, washiriki kumi walifanikiwa kutinga nusu fainali, Mtandao wa Al Kafeel Global uliripoti Jumamosi.

Hatimaye, wasomaji watatu kutoka kila kategoria walitangazwa kuwa washindi.

Katika kitengo cha Vijana, washindi walikuwa:

  1. Mohammed Abu Bakr kutoka Pakistani
  2. Ahmed Hassan Hamza kutoka Iraq
  3. Yasin Gholami kutoka Iran

Katika kitengo cha watu wazima, washindi walikuwa:

  1. Ahmed Jamal al-Rikabi kutoka Iraq
  2. Mahmoud El Sayed Abdallah kutoka Misri
  3. Mehdi Rahmatollah Taqipour kutoka Iran

Washindi hao walitunukiwa zawadi na Sayed Laith al-Mousawi, mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi wa Haram Takatifu ya Hadhrat Abbas AS

Tuzo ya Kimataifa la Kuhifadhi Qur’ani ya la Al-Ameed hutumika kama jukwaa la kukuza mazungumzo ya kimataifa ya Qur'ani na kuhumiza mashindano ya Qur'ani kieneo na kwingineko. Inaashiria pia dhamira ya  Haram ya Hadhrat Abbas AS katika kukuza sayansi, utamaduni, na maadili ya Qur'ani Tukufu katika jamii za Kiislamu.

/3487754

captcha