IQNA

Ahadi ya Kweli

Mchambuzi wa Syria: Operesheni ya Iran dhidi ya Israel imeleta mabadiliko ya kihistoria

10:28 - April 22, 2024
Habari ID: 3478715
IQNA - Mwanaharakati wa kisiasa wa Syria amesema shambulio la makombora ya Iran na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israeli mapema mwezi huu limeleta mabadiliko ya kihistoria.

Jafar Khazour aliandika katika makala kwamba operesheni ya Iran ilikuwa na nyanja na vipimo vingi, mojawapo ikiwa ni kujiondoa Iran kutoka kwenye hatua ya subira ya kimkakati hadi kwenye uzuiaji wa kimkakati.

Amesema operesheni hiyo ilikwamisha muongo mmoja wa juhudi za utawala wa Israel za kuzuia maendeleo ya uwezo wa harakati za mapamabno ya Kiislamu (muqawama) katika eneo la Asia Magharibi.

Kwa mtazamo wa kiutendaji, shambulio la Iran lilionyesha maendeleo makubwa ya kiteknolojia ambayo Iran imefikia, alisema.

Khazour ameongeza kuwa kwa mtazamo wa kistratijia operesheni hiyo immefungua mlango mpya wa kuporomoka utawala wa Kizayuni.

Operesheni hiyo iliyotekelezwa na Iran ilikuwa ni haki halali ya nchi hiyo na jibu linalofaa kwa mashambulizi ya kigaidi ya utawala wa Israel dhidi ya jengo la kidiplomasia la Iran nchini Syria, mchambuzi huyo alisisitiza.

Lilikuwa pia jibu la kibinadamu kwani makombora ya Iran hayakulenga vituo vyovyote vya kiraia au miundombinu, kulingana na Khazour.

Pia alibainisha kuwa kabla ya shambulio hilo dhidi ya Israel, Iran ilifanya juhudi za kimataifa kuhakikisha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaulaani utawala wa Israel kwa shambulio la Damascus lakini lilishindwa kuchukua msimamo sahihi.

Ameendelea kusema kuwa operesheni hiyo ya Iran ni uthibitisho wa nafasi amilifu ambayo Jamhuri ya Kiislamu inatekeleza katika kuunga mkono harakati za muqawama za eneo hili.

Mchambuzi wa Syria Anasema Operesheni ya Iran dhidi ya Israel ilikuwa ni mabadiliko ya kihistoria

3488023

Kishikizo: Ahadi ya Kweli
captcha