IQNA

Maualamaa Misri wakosolewa kutotangaza ISIS kuwa wakufurishaji

14:42 - January 13, 2016
Habari ID: 3470037
Mwanachama wa Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu Misri amewakosoa Maulamaa Misri kwa kutowatangaza magaidi wa kundi la Daesh au ISIS kuwa ni wakufurishaji.
Maualamaa Misri wakosolewa kutotangaza ISIS kuwa wakufurishaji

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tovuti ya Al Bawaba News imeandika katika hali ambayo Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar kinatambuliwa kama marejeo ya kidini kwa Waislamu wa madhehebu ya Sunni duniani ya Sunnia duniani, kituo hicho kimetumia visingizo kadhaa katika kutotangaza ISIS kuwa wakufurishaji.

Mohammad Al Jundi, mwanachama wa Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu Misri amesema: "Kundi la ISIS haliutambuia Uislamu na linaitumia dini hii kufikia malengo yake na hivyo umefika wakati wa kulitangaza rasmi kundi hili kuwa ni la wakufurishaji."

Ameongeza kuwa, Uislamu unasisitiza kuwa na rehema hata kwa wapinzani wa dini hii tukufu. Mwanazuoni huyo wa Misri ameongeza kuwa: "Uislamu haukubali lugha ya mauaji yasiyo na msingi wa kisheria kwani inaruhusia kuua tu wakati wa kujihami. Kile ambacho ISIS wanafana ni kwa maslahi ya nchi za Magharibi."

Al Jundi ameongeza kuwa vitendo vya ISIS ni nje ya duara la Uislamu na kwa hakika kundi hilo linakinzana na sheria za Kiislamu kwani sheria za Kiislamu zinasisitiza kustahamiliana na kuwatendea mema wazazi, mambo ambayo kundi la kigaidi la ISIS linapinga.

Hivi karibuni gaidi moja wa ISIS alimuua mama yake kwa sababu tu alikataa kufuata itikadi potovu za kundi hilo.

Katika upande mwingine Sheikh Nashat Zarii Imamu na Khatibu katika Wizara ya Awqaf Misri amewataka magaidi wa ISIS kuwa makafiri na kuongeza kuwa ni wadhifa muhimu wa maulamaa wa Kiislamu kukabiliana na fatwa batili za kundi hili. Hivi karibubuni Muhyiddin Afifi Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu Misri aliunga mkono hatua ya Al Azhar kutotangaza ISIS kuwa kundi la wakufurishaji kwa madai kuwa uamuzi huo utasaidia kutoenea ukufurishaji.

3466836
captcha