Kwa mujibu wa tovuti ya egynews.net, taarifa iliyotolewa Alhamisi na chuo hicho imelaani vikali mashambulizi
hayo yaliyofanywa na watu wenye silaha ambao baada ya kutekeleza hujuma
hizo walitoa vitisho dhidi ya Waislamu wa eneo hilo kuhakikisha wanahama
mara moja eneo hilo na kwamba watauawa endapo hawatofanya hivyo.
Taarifa hiyo mbali na kukitaja kitendo hicho kama uovu wa kuchupa
mipaka, pia imekitaja kuwa si cha ubinaadamu. Aidha taarifa hiyo ya
al-Azhar imesisitiza kuwa, dini Tukufu ya Uislamu inayovitambua vitendo
hivyo vilivyo kinyume na mafundisho ya dini hiyo na utu na ubinaadamu,
inavitaja kuwa ni kosa ambalo ni haramu kabisa. Imeyataka makundi ya
wabeba silaha kuheshimu matukufu ya kidini hususan nyumba za Mwenyezi
Mungu kama ambavyo imewataka Waislamu wa Iraq kujiepusha na kila aina ya
uchochezi wa kidini au njama zozote zenye lengo la kuigawa nchi hiyo.
Itakumbuwa kuwa siku ya Jumanne watu wenye silaha walishambulia kwa mabomu ya
moto misikiti saba na mamia ya maduka ya mji huo wa al-Miqdadiyah na
kuwaua watu wasiopungua 24. Magaidi wakufurishaji wa kundi la ISIS au Daesh wamejigamba kuhusika na hujuma dhidi ya misikiti hiyo.
3467292