Kwa mujibu wa tovuti ya KTimes, Sheikha Dhaan Saeed
Al Suraidi mwenye umri wa takribani miaka 82 kutoka kitongoji cha Adhan huko Ras al Kheima, Umoja wa Falme za
Kiarabu au Imarati, amehifadhi juzuu hizo za Qur'ani Tukufu na umri wake
haukuwa kizingiti.
Aidha pamoja na kuwa hajui kusoma wala kuandika, kwa
kutegemea irada yake iamra ameweza kujifunza
Qur'ani Tukufu.
Yeye ni ajuza mwenye ustadi na ambaye
anajishughulisha na ukulima wa kifugo na pia ni mtaalamu wa tiba ya miti
shamba.
Ummu Muhammad ameweza kuhifadhi Qur'ani kwa urahisi
kwa kutumia vifaa vya kidijitali vya kujifunza Qurani.
Akifafanua kuhusu namna alivyohifadhi Qur'ani
anasema: "Misi siwezi kusoma wala kuandika lakini chombo hiki cha
kidijitali ambayo kina uwezo wa kusoma aya za Qur'ani na kuzikariri nitakavyo
kimenisaidia sana na hivyo nimeweza kuhifadhi Qur'ani kwa njia sahali."
Bikizee huyo aidha amejisajili katika kituo cha
masomo ya Qur'ani katika eneo la Adhan ili aweze kuhifadhi juzuu zaidi za
Qur'ani. Halikadhalika ametangaza nia yake ya kushiriki katika mashidano ya
Qur'ani Imarati.
3470083