IQNA

Maulamaa wa Kishia Bahrain walalamikia ukandamizaji wa Utawala wa Aal Khalifa

19:27 - April 18, 2016
Habari ID: 3470253
Maulamaa wa madhehebu ya Shia nchini Bahrain wametoa taarifa na kulalamikia hatua ya utawala wa kifalme nchini humo kuwakamata maulamaa wa Kiislamu na maimamu wa misikiti.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika taarifa hiyo, maulmaa hao wamebainisha wasiwasi wao kuhusu hatua za kibaguzi za utawala wa Aal Khalifa na wameutaka utawala huo usitishe sera hizo za ukandamizaji.

Taarifa hiyo iliyotolewa Aprili 17 imesema: "Maulamaa wa Kishia hawataki kuibua fitina na hotuba wanazotoa misikitini ni kwa jaili ya masuala ya kidini na si kuchochea ghasia na misimamo mikali."

Hivi karibuni askari wa utawala wa kidikteta wa Bahrain wamemtia mbaroni Sheikh Muhammad al-Mansi, aalimu mashuhuri wa nchi hiyo kwa kosa la kusalisha Sala ya jamaa.

Mienendo ya kuwatia mbaroni masheikh na wanaharakati wa haki za binadamu nchini Bahrain ni sehemu ya siasa ambazo zimekuwa zikitekelezwa mara kwa mara na utawala huo wa kurithishana nchini Bahrain. Utawala huo unatekeleza siasa hizo za ukandamizaji kwa lengo la kuzima mapambano ya wananchi wa nchi hiyo dhidi ya dhulma na madikteta wa taifa hilo.

Hadi sasa maelfu ya wanaharakati na viongozi wa kidini akiwemo Sheikh Ali Salman, Katibu Mkuu wa harakati ya Kiislamu ya Al-Wifaq, wanaendelea kushikiliwa katika korokoro za utawala huo wa Bahrain mbele ya kimya cha jamii ya kimataifa. Hata hivyo na pamoja na ukandamizaji huo, maandamano dhidi ya utawala huo yameendelea kushuhudiwa katika maeneo tofauti ya utawala huo kibaraka wa Saudi Arabia.

3489621

captcha