IQNA

Utawala wa Bahrain wapiga marufuku Jumuiya ya Qur'ani

12:12 - June 20, 2016
Habari ID: 3470399
Utawala wa kiimla wa ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain umevuna Jumuiya ya Qur'ani nchini humo kwa madai kuwa eti imekiuka sheria.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Jameel Humaidan, Waziri wa Leba na Ustawi wa Jamii Bahrain amedai kuwa uamuzi wa kuvunja jumuiya hiyo umetegemea Kifungu cha 50 cha sheria ya mwaka 1989 kuhusu jumuiya kijamii na kiutamaduni.

Jumuiya hiyo imekuta ikifanya kazi ya kuchapisha na kusambaza nakala za Qur'ani bila malipo katika nchi mbali mbali duniani hasa zile ambazo Waislamu hawana uwezo wa kununua misahafu.

Jumuiya hiyo ilianzishwa mwaka 2006 na imekuwa ikitumia michango ya wafadhili kufanikisha shughuli zake zinazohusiana na uchapisha na usambazwaji nakala za Qur'ani Tukufu katika nchi za Afrika na Asia.

Wakuu wa Bahrain wameanzisha kampeni ya kukandamiza harakati za Kiislamu nchini humo kwa visingizio mbali mbali.

Siku ya Jumanne mahakama ya Bahrain ilibatilisha usajili cha vhama kikuu cha upinzani cha Al Wefaq na kuchukua duhibiti wa mali zake.

Katibu Mkuu wa Al Wefaq alifungwa gerezani Desemaba mwaka 2014 kwa madai eti alijaribu kuupindia utawala wa kifalme kwa msaada wa kigeni, tuhuma ambazo amekanusha.

Tokea Februari mwaka 2011, Bahrain imekuwa ikishuhudia mwamko wa Kiislamu ambapo wananchi wanataka kuwa na haki ya kuwachagua viongozi na kuwepo usawa na uadilifu katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi. Utawala Bahrain, ambao ni muitifaki mkubwa wa Marekani na Uingereza, umekuwa ukikandamiza maandamano ya ambani ambapo idadi kubwa ya watu wameuawa, mamia kujeruhiwa na wengine wengi kushikiliwa gerezani.

3460143

captcha