IQNA

Waandamanaji Berlin

Saudi Arabia ni Benki ya Daesh (ISIS)"

19:09 - May 15, 2016
Habari ID: 3470314
Maandamano yamefanyika nje ya Ubalozi wa Saudi Arabia mjini Berlin, Ujerumani ambapo washiriki wameilaani Saudia kwa kuendelea kutoa misaada kwa kundi la kigaidi la Daesh au ISIS.
Waandamanaji hao waliokuwa na hasira wamelaani uungaji mkono wa Saudia kwa magaidi huko Syria, Iraq, Yemen na nchi zingine duniani.
Katika kuonyesha namna Saudi Arabia inavyounga mkono makundi ya kigaidi ikiwemo ISIS, waandamanaji hayo ambao wameandamana usiku wa jana walitumia mwangaza wa laser kuibua bendera ya kundi la kigaidi la ISIS na juu yake ikiwa na maneneo ya 'Benki ya Daesh' na kuelekeza mwangaza huo katika jengo la ubalozi wa Saudia mjini Berlin.
Maandamano hayo ni ishara ya wazi kuwa waliowengi barani Ulaya wanaamini kuwa utawala wa Saudia ni muungaji mkono mkuu wa makundi ya kigaidi. Serikali ya Syria kwa mara kadhaa imeituhumu Marekani na waitifaki wake Mashariki ya Kati kama vile Uturuki, Qatar, Saudi Arabia kuwa ni waungaji mkono wakuu wa magaidi nchini humo. Viongozi wa Iraq pia wanasema wana ushahidi kuwa Saudi Arabia inawaunga mkono magaidi wa ISIS nchini humo.
captcha