IQNA

Mkuu wa Kituo cha Haki za Binadamu Bahrain akamatwa, Masheikh marufuku kuwa wanasiasa

10:50 - June 13, 2016
Habari ID: 3470381
Katika kuendelea ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Bahrain, wanajeshi wa utawala wa Aal Khalifa wamemtia mbaroni Nabil Rajab, mkuu wa kituo cha haki za binadamu nchini humo.
Kwa mujibu wa Samia Rajab, mkewe Nabil Rajab,  wanajeshi  wa utawala wa kiimla wa ukoo wa Aal Khalifa walihujumu nyumba yao ni kumkamata mtetezi huyo wa haki za binadamu. Nabil Rajab ametia mbaroni mara kadhaa tokea mwamko wa Kiislamu uanze katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi mwaka 2011.
Nabil ,ambaye pia ni mwanzilishi ya Kituo cha Haki za Binadamu cha Ghuba ya Uajemi, amekuwa mkosoaji mkubwa wa ukandamizaji na ukatili unaotumiwa na utawala wa Aal Kalifa kuzima maandamano ya amani ya wananchi.

Kwingineko , mfalme wa Bahrain ametoa dikrii ya kubadilishwa baadhi ya vipengee vya kisheria kuhusu vyama vya kisiasa.

Mfalme Hamad bin Issa Aal Khalifa ametoa dikrii ya kubadilishwa baadhi ya vipengee vya kisheria kuhusu vyama vya kisiasa na kupiga marufuku shughuli za siasa zinazoendeshwa na vituo vya kidini na wanazuoni nchini humo.

Kwa mujibu wa dikrii hiyo, ni marufuku huko Bahraini kutumiwa mimbari za kidini na hotuba kwa ajili ya shughuli za kisiasa na kuwa na uhusiano na maafisa wa vituo vya kidini na vyama vya kisiasa.

Wakati huo huo vikosi vya usalama vya utawala wa Aal Khalifa hadi sasa vimewatia mbaroni maulamaa wengi kwa sababu tu ya kuzungumzia masuala ya kisiasa ma kijamii katika hotuba za Swala ya Ijumaa.

Bahrain imekuwa ikishuhudia maandamano ya amani ya raia wa nchi hiyo tangu mwaka 2011 dhidi ya utawala ulioko madarakani wa ukoo wa Aal Khalifa. Wananchi wa Bahrain wanataka kuwa huru, kutendewa uadilifu, kukomeshwa vitendo vya kibaguzi na kuingia madarakani serikali halali ya kidemokrasia.
3460076


captcha