IQNA

Wabunge Ulaya walaani kukandamizwa Waislamu Warohingya nchini Myanmar

19:03 - July 08, 2016
Habari ID: 3470438
Bunge la Umoja wa Ulaya limelaani vikali kuendele akukandamiwa Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika taarifa walioyotoa Alhamisi, wabunge hao wametaka serikali ya Myanmar iwaruhusi mara moja na bila pingamizi wakaguzi wa Umoja wa Mataifa, waandishi habari, na mashirika ya kutetea haki za binadmau aktika jimbo la magharibi mwa nchi hiyo la Rakhine ambalo lina Waislamu wa kabila la Rohingya120,000 waliofukuzwa makwao na ambao wanaishi katika kambi 30.

Wakati huo huo Kamisheni ya Kiislamu ya Haki za Binadamu yenye makao yake London nchini Uingereza (IHRC) imesema kuwa kutokuwepo mashinikizo ya kimataifa ndiyo sababu ya kuendelea mateso na ukandamiza wa mabudha wenye misimamo mikali dhidi ya Waislamu nchini Myanmar.

Mwananchama wa kamisheni hiyo, Arzu Merali amesema ukosoaji hafifu wa jumuiya za kimataifa kuhusu dhulma wanazofanyiwa Waislamu wa Myanmar hauna taathira yoyote na kwamba kimya cha jamii ya kimataifa kuhusu ukatili unaofanywa dhidi ya Waislamu wa Myanmar ni miongoni mwa sababu kuu za mgogoro huo.

Merali amesema kuwa, jamii ya kimataifa haijachukua hatua yoyote ya kivitendo ya kuishinikiza serikali ya Myanmar na kwa msingi huo watawala wa nchi hiyo hawaoni sababu ya kubadili sera na siasa zao kuhusu jamii ya Waislamu wa nchi hiyo.

Mwanachama huyo wa Kamisheni ya Kiislamu ya Haki za Binadamu amesema kuwa, madola makubwa hususan Marekani yanafuatilia maslahi yao na kwamba yamenyamazia kimya mauaji na mateso ya Waislamu wa Myanmar kwa sababu hayagusi maslahi ya nchi hizo.

Maelfu ya Waislamu wa Myanmar wameuawa na malaki ya wengine kulazimika kuwa wakimbizi kutokana na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Madhudha wenye misimamo mikali dhidi ya jamii ya Waislamu wa Rohingya.

Serikali ya Myanmar inakataa kuwatambua Waislamu Warohingya kuwa raia na inawataja kuwa ni wahamiaji haramu.

3460324

captcha