IQNA

Mwanamke Mwislamu adhalilishwa Uingereza kwa sababu ya kusoma kitabu kuhusu Syria

22:04 - August 04, 2016
Habari ID: 3470494
Mwanamke Mwislamu aliyekamatwa Uingereza kwa kusoma kitabu kuhusu Syria ameazimia kuwasilisha kesi kulalamikia namna alivyo dhalilishwa na wahudumu wa ndege pamoja na askari wa kupambana na ugaidi.

Faizah Shaheen, ambaye kutokana na kusoma kitabu kinachozungumzia tasnia ya Syria ndani ya ndege, alitiwa mbaroni na polisi ya Uingereza na kuhojiwa, amesema kuwa atawashitaki polisi na wahudumu wa ndege hiyo.

Sheheen ambaye ni mfanyakazi katika taasisi ya tiba ya kitaifa nchini Uingereza alitiwa mbaroni mwezi Julai mwaka huu wakati alipokuwa ndani ya ndege akitokea Uturuki kuelekea mji wa Doncaster, Uingereza. Inaelezwa kuwa akiwa ndani ya ndege muhudumu mmoja alitoa taarifa kwa polisi ambapo baada ya ndege hiyo kutua alitiwa mbaroni na polisi hao na kuanza kumuhoji kwa muda baada ya kushikiwa kuwa ni gaidi kutokana na kusoma kitabu chenye jina linalosema: 'Syria Speaks: Art and Culture from the Frontline' yaani 'Syria Yazungumza: Sanaa na Utamaduni Katika Medani ya Vita.'

Mkuu wa kamisheni ya masuala ya ndani katika bunge la Uingereza, ametoa tamko kuhusiana na kitendo hicho huku akiwataka wahudumu wa ndege kumuomba radhi mwakamke huyo. Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwepo na wimbi kubwa la chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu barani Ulaya kutokana na hujuma za kundi la kigaidi la ISIS.

3520124



captcha