IQNA

Utawala wa Bahrain wazuia sala ya Ijumaa ndani ya msikiti

23:05 - August 05, 2016
Habari ID: 3470496
Utawala wa kiimla wa Bahraini umetumia askari kuwazuia Waislamu kutekeleza ibada ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Imam Sadiq (AS) katika kijiji cha Diraz nje ya mji mkuu Manama.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, askari wa utawala wa ukoo wa Aal Khalifa wamewazuia Waislamu kusalia Swala ya Ijumaa katika kijiji hicho ambacho aghalabu wa wakazi wake ni Waislamu wa madhehebu ya Shia. Baada ya kila mmoja kuswali kivyake, yaani furada, waumini walimiminika mabarabarani katika maandamano dhidi ya utawala huo wa kifalme.

Waandamanaji wamelaani dhulma na ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Aal-Khalifa dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo.

Waandamanaji hao wamesikika wakipiga nara za kumlaani Mfamle Hamad bin Isa Al Khalifah wa nchi hiyo kwa namna anavyoiendesha nchi kwa mkono wa chuma. Aidha waandamanaji hao walikuwa wamebeba mabango yenye picha za mwanachuoni mashuhuri wa Kishia nchini humo Sheikh Isa Qassim.

Hii ni mara ya tatu kwa watawala wa Manama kuzuia Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Imam Sadiq katika kijiji cha Diraz. Julai 22, maafisa usalama nchini Bahrain walizuia Swala ya Ijumaa katika msikiti huo sambamba na kuwatia mbaroni watu 50 katika kijiji hicho, kaskazini magharibi mwa nchi.

Wananchi wa Bahrain wamekuwa wakifanya maandamano ya kupinga kuvuliwa uraia Sheikh Isa Qassim kwa tuhuma zisizo na msingi kuwa eti anachochea malumbano ya kimadhehebu na ghasia licha ya kuwa mwanachuoni huyo ni mashuhuri kwa misimamo yake ya kutetea Umoja wa Kiislamu na maandamano ya amani Bahrain.

Malalamiko na maandamano ya wananchi wa Bahrain dhidi ya watawala dhalimu wa nchi hiyo yamekuwa yakiendelea tokea tarehe 14 Februrai 2011. Tokea mwanzoni mwa maandamano hayo watawala wa ukoo wa Aal Khalifa wamekuwa wakitekeleza mbinu tofauti za kupambana na wapinzani.

3520219

captcha