IQNA

Bahrain yamzuia mwanaharakati wa haki za binadamu

13:18 - August 23, 2016
Habari ID: 3470536
Utawala wa kiimla wa Bahrain umemzuia mwanaharakati wa haki za binadamu kuondoka nchini humo ili kwa kuhofia kufichuka rekodi mbaya ya haki za binaadamu katika ufalme huo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Enas Oun ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Uwekazji Nyaraka katika Kituo cha Haki za Binadamu Bahrain, alisimamishwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Bahrain siku ya Jumatatu wakati akielekea katika warsha ya haki za binadamu nchini Tunisia. Maafisa wa usalama wamedai kuwa mwanaharakati huyo hana ruhusa kusafiri kutokana na uchunguzi wa jinai dhidi yake.

Wakati huo huo shirika la pamoja la kutetea haki za binadamu na demokrasia la Bahrain na Ujerumani limeripoti kuwa utawala wa Aal Khalifa umewaita kuwasaili maulamaa 70 wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo.

Shirika hilo limesema madai ya utawala wa Aal Khalifa kwamba linaheshimu haki za binadamu ni dhihaka tupu na kubainisha kwamba katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita maafisa wa utawala huo wamewaita kuwasaili na kuwahoji maulamaa 70 wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia, wamewatia nguvuni maulamaa wengine 20, washairi tisa na zaidi ya wanaharakati 50 wa kisiasa; na kwamba hatua hizo ni ithbati ya ukweli wa taarifa ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu dhulma wanazotendewa Waislamu wa Kishia nchini Bahrain.

Shirika hilo aidha limetoa wito kwa utawala wa Aal Khlifakusimamisha mara moja mashambulio na hujuma dhidi ya raia wa madhehebu ya Shia, kuheshimuhaki zao za kiraia, kisiasa na kijamii na kujiepusha na hatua za kuchochea hitilafu za kimadhehebu nchini humo.

Malalamiko na maandamano ya wananchi wa Bahrain dhidi ya watawala dhalimu wa nchi hiyo yamekuwa yakiendelea tokea tarehe 14 Februrai 2011. Tokea mwanzoni mwa maandamano hayo watawala wa ukoo wa Aal Khalifa wamekuwa wakitekeleza mbinu tofauti za kupambana na wapinzani.

3460792

captcha