IQNA

Binti Muirani mwenye umri wa miaka 9 katika mashindano ya Qurani Imarati

21:50 - November 04, 2016
Habari ID: 3470650
IQNA-Binti Muirani mwenye umri wa miaka 9, Hannaneh Khalfi yuko katika Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE (Imarati) kushiriki mashindano ya Qur’ani ya wanawake.

Akizungumza na mwandishi wa IQNA, baba yake Hannaneh, Bw. Mustafa Khalfi amesema bintiye yuko Imarati akiwa ameandamana na mama yake. Ameongeza kuwa, Hannaneh amekuwa akijitayarisha kwa muda wa miezi miwili kwa ajili ya mashindano hayo ya kimataifa ya kuhifadhi Qur’ani ya Imarati. Amesema kila siku amekuwa akisoma Juzuu tatu za Qur’ani na pia amekuwa akiulizwa maswali ya juzuu 10 kila siku katika kujitayarisha kwa ajili ya mashindano hayo.

Bw. Khalfi amesema hii ni mara ya kwanza kwa Hannaneh kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu na kuongeza kuwa ana matumaini kuwa binti yake anaweza kuchukua nafasi ya kwanza katika mashindano hayo ya Imarati.

Duru ya Kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Sheikha Fatima Bint Mubarak yatafanyika kuanzia Novemba 6-18 mjini Dubai. Kuna washiriki 70 wa kike waliohifadhi Qur’ani kutoka nchi 72 za Kiarabu, Afrika, Amerika ya Latini, Asia na Ulaya  ambao watashiriki katika mashindano hayo ya kuhifadhi Qur’ani maalumu kwa wanawake.

Washiriki ni kutoka umri wa miaka 9 hadi 23 ambapo washindi wa nafasi za kwanza, pili na tatu watapata zawadi za fedha taslimu AED 250,000; AED 200,000; na AED 150,000 kwa taratibu.Binti Muirani mwenye umri wa miaka 9 katika mashindano ya Qurani UAE

Mashindano hayo ni sehemu ya mashindano ya Qur’ani yajulikanayo kama Zwadi ya Kimatiafa ya Qur’ani Tukufu ya Dubai ambayo hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

3543253

captcha