IQNA

Mashindano ya Qur’ani Amerika Kaskazini kufanyika Toronto

23:35 - December 21, 2016
Habari ID: 3470752
IQNA-Awamu ya 12 ya Mashindano ya Kila Mwaka ya Qur’ani ya Amerika Kaskazini yamepangwa kufanyika mjini Toronto, Canada mwaka 2017.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yaandaliwa na Waqfu wa Kiislamu wa Torotno na yatakuwa na vitengo viwili tafauti ya wasichana na wavulana.

Mashindano ya wanawake yamepangwa kufanyika Februari 25 na yale ya wavulana yatafanyika Machi 10-12.

Tayari mashindano ya mchujo yameshafanyika na wale waliofuzu kushiriki katika mashindnao hayo makuu wameshajulishwa.

Kategoria za mashindano hayo zitajumuisha qiraa na kuhifadhi Qur’ani tukufu katika vitengo tafauti na kwa ajili ya makundi mbali mbali ya umri.

3461718

captcha