IQNA

Iran kuandaa mashindano ya Qur'ani ya wenye ulemavu wa macho

14:01 - January 18, 2017
Habari ID: 3470803
IQNA-Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeandaa mashindano ya pili ya kimataifa ya Qur'ani ya watu wenye ulemavu wa macho.
Iran kuandaa mashindano ya Qur'ani ya wenye ulemavu wa macho

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yemepangwa kufanyika mjini Tehran kuanzia Aprili 19-26 na yatajumuisha kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu na pia kusoma Qur'ani Tukufu.

Kwa sasa mashindano hayo ni ya wanaume pekee.

Kwa mujibu wa kamati andalizi, wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo wanapaswa kutimiza masharti yafuatayo:

1.Mshirikia anapaswa kuwa raia wan chi ambayo imemtuma kushiriki katika mashindano.

2. Mshiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Iran mwaka jana hawawezi kushiriki mashindano ya mwaka huu.

3. Mshiriki anapaswa kuwa na uwezo wa kusoma Qur'ani kwa kuzingatia misingi na kanuni za Tajweed, Sawt na Lahn.

4. Kila mshiriki anaweza kushindana katika kategoria moja tuu, ima ya kuhifadhi au kusoma.

5. Kila nchi inaruhusiwa kuwa na mtu moja atakayeambatana na mshiriki au washiriki.

6. Kamati andalizi itagharamia gharama za visa,tiketi za ndege, malazi na sehemu ya kulala wa washiriki na msaidizi moja wa kila nchi.

7. Nyaraka zinazotakikana kwa washiriki kabla ya kusafiri ni

A. Kopi ya ukurasa wa kwanza wa pasi ya kusafiria au pasipoti

B. Picha mbili za pasipoti

C. Fomu iliyojazwa ya washiriki

8. Tarehe ya mwisho ya kuwasilisah ombi la kushiriki ni Februari 3, 2017.

9.Kwa maelezo zaidi kuhusu mashindano na kanuni tafadhali tembele ukurasa wa intaneti wa www.quraniran.ir au wasiliana na kamati andalizi kupitia nambari zifuatazo

Simu: 0098-922-3784093

Fax : 0098-21-64872627

Email: awqafiraq@yahoo.com

http://iqna.ir/en/news/3461961/

Kishikizo: iran
captcha