IQNA

Watalii Waislamu kupata huduma Halal nchini Kenya

13:54 - February 04, 2017
Habari ID: 3470832
IQNA-Kenya imeanzisha mkakati wa huduma za 'Halal' za kitalii kwa ajli ya ongezeko la watalii Waislamu nchini humo.

Halmashauri ya Kuratibu Utalii nchini Kenya TRA  imesema imeandaa sheria za kutoa vibali vya 'Halal' kwa ajili maeneo ya kitalii yanayolenga kuwahudumia watalii Waislamu wanaotaka huduma kwa msingi wa mfundisho ya Kiislamu.

Wakuu wa utalli nchini Kenya wanasema, idadi ya watalii Waislamu wanaofika nchini Kenya inazidi kuongoezeka. Kwa mfano mwaka 2015, Kenya ilipokea watalii 40,874 kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE, katika hali ambayo idadi hiyo ilikuwa 24,828 mwaka 2014.

Mkurugenzi Mkuu wa TRA  Lagat Kipkorir amesema viwango vya utalii Halal vinatayarishwa kwa ushuhirikiano na Idara ya Viwango Kenya. "Tumetayarisha mpango wa kina kutunga kanuni, kuwashirikisha washikadau, kudhamini viwango, na mafunzo kabla ya kuzindua rasmi utalii Halal," amesema Kipkorir.

Halikadhalika amesema watalii Waislamu wana matakwa maalumu kwa kuzingatia umri na utaifa na kwamba kuna haja ya kuwepo miongozo maalumu kuhakikisha sheria za Kiislamu zinazingatiwa katika chakula, mahala pa kulala na pia katika makongamano.Watalii Waislamu kupata huduma Halal nchini Kenya

Aidha amesema mashauriano yanaendelea kuhusu kukamilisha mchakato huo wa kuanzisha huduma Halal za kitalii nchini humo. Ameongeza kuwa mchakato huo utapata msukumo katika Mkutano ya Kimataifa wa Halal utakaofanyika nchini Kenya baadaye mwaka huu. Kipkorir amesema kwa mujbu wa ratiba iliyopo, utalii Halal nchini Kenya utazinduliwa mapema mwaka 2018.

Kwa ujumla katika maeneo yenye kutoa huduma za kitalii Halal kwa ajili Waislamu kwa kawaida huwa hayana pombe, kuna sehemu tafauti za kuogolea za wanaume na wanawake na mfumo mzima wa upishi huzingatia kikamilifu chakula halali. 

Hivi karibuni pia Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alisaini sheria itakayoimarisha nafasi ya Kenya kama kitovu cha mfumo wa fedha wa Kiislamu barani Afrika.

Mwezi Oktoba mwaka jana serikali ya Kenya ilizindua ofisi maalumu ijulikanayo kama Kurugenzi ya Mradi wa Kifedha wa Kiislamu (PMO) itakayoongozwa na Shirika la Kimataifa la Kutoa Ushauri na Dhamana Kuhusu Huduma za Kifedha za Kiislamu (IFAAS).

3570143
captcha