IQNA

Huenda Sheikh Zakzaky akawa kipofu akiwa kizuizini

19:56 - February 14, 2017
Habari ID: 3470849
IQNA: Harakati ya Kiislamu Nigeria (INM) imetahadharisha kuwa kiongozi wa harakati hiyo, Sheikh Ibrahim Zakzaky huenda akapoteza uwezo wa kuona na kuwa kipofu akiwa kizuizini.

Katika taarifa, msemaji wa harakati hiyo Ibrahim Musa amesema, madaktari wanaomshughulikia Sheikh Zakzaky ambaye anashikiliwa kinyume cha sharia wamesema tayari wamesahwafahamisha maafisa wa serikali kuwa yamkini mwanazuoni huyo wa Kiislamu akapoteza kikamilifu uwezo wa kuona iwapo hatapata matibabu yanayofaa haraka iwezekanavyo.

Bw. Musa amesema serikali ya Nigeria imechukua hatua ya makusudi ya kumuua Sheikh Zakzaky kwa kumnyima matibabu kwani hivi sasa hali yake jumla ya kiafya si nzuri. Msemaji wa Harakati ya Kiislamu Nigeria ametoa wito kwa Wanigeria kumsaidia Sheikh Zakzaky ambaye anashikiliwa pamoja na mke wake. Aidha INM imeitaka jamii ya kimataifa imuwajibishe Rais Muahmmadu Buhari wa Nigeria na wale wote waliohusika katika mauaji ya umati ya Waislamu katika mji wa Zaria. Halikadhalika ameitaka serikali itii amri ya mahakama na kumuachilia huru Sheikh Zakzaky mara moja.

Itakumbukwa kuwa Sheikh Ibrahim Zakzaky akiwa na mke wake alitiwa mbaroni na Jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka 2015 katika kituo cha kidini huko katika mji wa Zaria jimboni Kaduna. Tokea wakati huo Sheikh Zakzaky na mkewe wamekuwa wakizuiliwa katika mojawapo ya vituo vya kijeshi vya nchi hiyo bila kufunguliwa mashktaka.

Jeshi hilo lilidai kuwa wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria walikuwa na njama ya kutaka kumuua Mkuu wa Jeshi la Nigeria, madai ambayo yamekanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo.

Jeshi hilo katili liliizika miili ya waliouawa katika kaburi moja kwa lengo la kuficha ushahidi wa ukubwa wa jinai hiyo. Inakadiriwa kuwa Waislamu 1000 wasio na hatia waliuawa katika tukio hilo huku Sheikh Zakzaky, ambaye hali yake ya kiafya si nzuri, akiendelea kushikiliwa korokoroni pasina kufunguliwa mashtaka.

3470815

captcha