IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Vyombo vya Mahakama Iran vimtetee Sheikh Zakzaki na Waislamu wa Myanmar, Kashmir

11:24 - July 04, 2017
Habari ID: 3471049
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran ametaka vyombo vya mahakama nchini viwatetee Waislamu wanaodhulumiwa duniani

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo wakati alipoonana na mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran Ayatullah Sadeq Amoli Larijani na maafisa wengine wa mahakama nchini.

Amesema, ni muhimu kwa Vyombo vya Mahakama Iran kufuatilia masuala tofauti ya kimataifa katika upeo wa kisheria.

Amesisitiza kuwa, Vyombo vya Mahakama Iran vinapaswa kutoa msimamo katika masuala kama vile vikwazo vinavyowekwa dhidi ya Iran, kutaifishwa na Marekani mali za Iran, ugaidi na kuunga mkono shakhsia wanaodhulumiwa duniani kama vile Sheikh Ibrahim Zakzaki, mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria au kutangaza uungaji mkono wake kwa Waislamu wa Myanmar na Kashmir. Amesema kufuatilia mambo kama hayo katika upeo wa kisheria na kutangaza uungaji mkono au upinzani wake mkali kwa matukio ya kimataifa kunapaswa kuakisiwa ulimwenguni.

Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, ni jambo la dharura kuchunga neema za Mwenyezi Mungu na kutoa mfano wa baadhi ya neema hizo kwa kusema: "neema ya kuwepo vijana" "neema ya Jamhuri ya Kiislamu" "neema ya kuwa na Vyombo vya Mahakama na nguvu zake" na neema ya kuwekouungaji mkono, mapenzi na utiifu wa wananchi kwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran" ni miongoni mwa neema kubwa za Mwenyezi Mungu ambazo watu wote humu nchini wanapaswa kuzichunga nawahakikishe hawazipotezi, bali wazitumie kwa njia bora kabisa.

3463260

captcha