IQNA

Daktari atarajia kuwa gavana wa kwanza Mwislamu Marekani

19:36 - March 03, 2017
Habari ID: 3470875
IQNA: Daktari mwenye umri wa miaka 32 anatarajia kuwa Mwislamu kwa kwanza gavana nchini Marekani baada ya kutangaza nia ya kugombea ugavana wa jimbo la Michigan.

Abdulrahman Mohamed El-Sayed alizaliwa mwaka 1985 katika Kaunti ya Gratiot jimboni Michigan na wazazi ambao walihamia Marekani kutoka Misri. Daktari huyo ni mashuhuri kwa mafanikio na kujitolea kwake kurekebisha idara ya afya jimboni Michigan.

Daktari El-Sayed aliteuliwa na Meya wa Michigan Mike Duggan kuwa Afisa Mkuu wa Afya na Mkuregenzi Mtendaji wa Idara ya Afya ya Detroit mwaka 2015 na hivyo kuwa kamshina mchanga zaidi wa afya katika mji mkubwa nchini Marekani. Wakati akitangaza uamuzi wake wa kugembea ugavana Daktari El-Sayed alisema: "Nagombea kwa sababu naamini nitakuwa gavana bora zaidi katika jimbo la Michigan-niwe au nisiwe Mwislamu. Imani yangu ni muhimu kwangu kama amabvyo ni muhimu kwa Wamarekani na Wamichigan."

Amesisitiza kuwa, maadili ya Kiislamu mhimili mkuu katika kazi zake kama mtumishi wa umma lakini akaongeza kuwa, kipaumbele chake cha kwanza ni kuwahudumia watu wa Michigan.

Iwapo atacahguliwa, si tu kuwa Daktari El-Sayed atakuwa gavana wa kwanza Mwislamu Marekani bali pia atakuwa gavana mwenye umri wa chini zaidi Marekani tokea rais wa zamani Bill Clinton alipochaguliwa gavana wa Arkansas mwaka 1978.

Daktari huyo alihitimu Chuo Kikuu cha Tiba cha Michigan na kisha kupata Shahada ya Uzamili (MA) katika Chuo Kikuu cha Columbia kabla ya kupata Shahada ya Uzamifu katika uga wa afya ya jamii kutoka Chuo Kikuu cha Oxford.

Huenda El-Sayyed akapata matatizo katika kampeni zake kufuatia ongezeko kubwa la chuku dhidi ya Uislamu na Waislamu Marekani. Uchaguzi wa ugavana wa jimbo la Michigan umepangwa kufanyika Novemba 6. 2018.

3580149

captcha