IQNA

Utawala dhalimu wa Bahrain waakhirisha tena kesi ya Sheikh Qassim

20:41 - March 14, 2017
Habari ID: 3470895
IQNA-Utawala dhalimu wa Bahrain umeakhirisha tena hukumu dhidi ya Ayatullah Sheikh Isa Qassim, mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu nchini humo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, hukumu dhidi ya kiongozi huyo wa Kiislamu ilipangwakutolewa leo Jumanne lakini sasa imeakhirishwa hadi Mei 7.

Hayo yanajiri wakato ambao jana Jumatatu Maulamaa wa Kiislamu nchini Bahrain walitoa taarifa na kusema, ni wadhifa wa kidini na kitaifa kumtetea Sheikh Qassim, kiongozi wa kimaanawi wa harakati wa mapinduzi ya wananchi.

duru za habari zimedokeza kuwa, utawala wa Manama unapanga kumpeleka uhamishoni nchini Uturuki Sheikh Isa Qassim, kwa lengo la kupunguza taharuki na ghadhabu za wananchi wanaoishinikiza serikali kumuachiahuru mara moja.

Katika taarifa Maulamaa wameongeza kuwa kuwa, "Leo Bahrain imefika katika kipindi ambacho, madhalimu na maadui wameungana pamoja kwa ajili ya kuwahujumu wananchi, dini, madhehebu na viongozi wawa kidini."

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, taifa la Bahrain lenye kupambana na kusimama kidete linaweza kujisimamia hata katika hali ngumu zaidi na litaendeleza mapambano hadi kupata ushindi mbele ya mfumo wa kibaguzi wa ukoo wa Aal Khalifa.

Kesi ya Sheikh Qassim imekuwa ikiakhirishwa mara kwa kutokana na hofu ilionao utawala wa Aal Khalifa kuhusu majibu makali ya wananchi endapo mwanazuoni huyo maarufu wa Kiislamu atahukumiwa.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain inadai kuwa Sheikh Issa Qassim anahudumia madola ajinabi na kuibua hitilafu za kimadhehebu na kwa msingi huo Juni 20 mwaka jana ulimpokonya uraia.Sheikh Qassim amekanusha tuhuma hizo na kuzitaja kuwa zisizo na msingi.

Duru za habari zimedokeza kuwa, utawala wa Manama unapanga kumpeleka uhamishoni nchini Uturuki Sheikh Qassim, kwa lengo la kupunguza taharuki na ghadhabu za wananchi wanaoishinikiza serikali kumuachiahuru mara moja.

Tokea tarehe 14 Februari mwaka 2011, Bahrain imekuwa ikishuhudia harakati ya mwamko wa Kiislamu ambapo wananchi wanataka kuwa na haki ya kuwachagua viongozi wao na kuwepo usawa na uadilifu katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.

3584083

captcha