IQNA

Nakala za Qur'ani zapasuliwa msikitini Marekani

15:53 - March 18, 2017
Habari ID: 3470900
TEHRAN (IQNA)-Mtu asiyejulikana ameuhujumu msikiti nchini Marekani katika jimbo la Arizoni mjini Tucson na kupasua nakala kadhaa za Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Kituo cha Kiislamu cha Tucson kimetoa taarifa na kusema kamera za usalama zimeonyesha mwanaume aliyekuwa amevalia T-sheti ya Chuo Kikuu cha Arizon, akiingia katika msikiti saa tisa unusu alfajiri Jumatatu na kiwa hapo alipasua nakala kadhaa za Qur'ani huku akizurusha huku na kule katika ukumbi wa sala kabla ya kuondoka.

Taarifa hiyo imesema hakuna yeyote aliyejeruhiwa katika hujuma. Aidha taarifa hiyo imesema taswira zilizonaswa katika kamera za usalama zinaonyesha mvamizi huyo alikuwa na lengo la kuharibu mali za kituo hicho cha kidini. Maafisa wa usalama katika Idara ya Polisi ya Tucson wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Kufuatia tukio hilo, Bw. Imraan Siddiqui, mkuregenzi mtendaji wa tawi la Arizona la Baraza la Uhusiano wa Uislamu na Marekani ,CAIR, ametoa wito kwa maafisa wa usalama katika eneo hilo kuhunguza hujuma hiyo ili wabaini iwapo chanzo hake ni uhalifu wa kawaida au chuki za kidini. Aidha amewataka viongozi wa kidini na kisiasa kuzungumza kuhusu ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu katika jimbo hilo.

Baada ya ushindi wa Trump na kuapishwa kwake Januari 20 kumeshuhudiwa hujuma dhidi ya misikiti na vituo vya Kiislamu Marekani na pia katika nchi jirani ya Canada.

Mwezi moja baada ya ushindi wa Trump katika uchaguzi wa rais Marekani mnamo Novemba 8 mwaka jana, Shirika la Southern Povert Law Centre (SPLC) lilirekedi vitendo 1,098 vya chuki kote Marekani ambapo idadi kubwa ya waliotekeleza vitendo hivyo walimtaja Trump na nara yake ya Kuifanya Marekani Kuwa na Nguvu Tena (Make America Great Again) au matamshi yake dhidi ya wanawake.

Kwa mujibu Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani ambalo hutetea haki za Waislamu, mbali na misikiti na vituo vya Kiislamu kushambuliwa pia wanawake na watoto Waislamu wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu.

3462421
captcha