IQNA

Kinara wa ISIS, al-Baghdadi, amezingirwa huko Mosul, Iraq

12:34 - April 03, 2017
Habari ID: 3470916
TEHRAN (IQNA) Duru za usalama Iraq zinadokeza kuwa kuna uwezekano kuwa, kinara wa kundi la ISIS au Daesh la magaidi wakufurishaji kundi, Abubakar al-Baghdadi amenaswa kwenye mzingiro uliowekwa kwenye katika mji Mosul nchini Iraq.

Taarifa zinasema takribani siku kumi zilizopita magaidi wa ISIS wakiwa na magari yapatayo arubaini na kusindikizwa na vifaru kadhaa walijaribu kuingia eneo la Tala'far lililoko kwenye barabara inayoishia mjini Mosul wakitokea nchini Syria.

Duru hiyo ya Iraq imeongeza kuwa magaidi hao walijaribu kuuvunja mzingiro wa eneo hilo, na ili kuimarisha ngome zao wakajaribu kujiunga na magaidi wengine walioko kwenye mzingiro wa Tala'far kwa ajili ya kufungua njia ya Mosul, lakini vikosi vya kujitolea vya wananchi viliwaangamiza magaidi hao wote.

Wakati huohuo jeshi la Iraq limetangaza kuwa operesheni ya kuukomboa mji wa Mosul imesimamishwa kwa sababu ya kulinda maisha ya raia na kwa ajili ya kufungua vivuko salama vya kupita raia hao katika eneo hilo. Hivi sasa mapigano yamekita kwenye eneo la kandokando ya msikiti wa Jamia wa An-Nuri magharibi mwa Mosul, mahala ambapo yapata miaka mitatu nyuma kinara wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la ISIS Abubakar al-Baghdadi alitangaza kila alichodai kuwa eti ni dola la Kiislamu. Aidha al Baghdadi ambaye jina lake asili ni Ibrahim al Sammarai alikuwa ameutangaza mji wa Mosul kuwa mji mkuu wa hiyo khilafa yake nchini Iraq na kwa msingi huo kukombolewa mji huo kutakuwa ni pigo kubwa kwa kundi hilo la kigaidi.

Magaidi wa ISIS wamekuwa wakiendesha kampeni ya mauaji ya kinyama nchini Iraq na Syria tokea mwaka 2014. Kundi hilo lenye itikadi za Kiwahhabi, ambalo linapata himaya ya siri na ya wazi kutoka baadhi ya nchi za Magharibi, utawala wa Kizayuni wa Israe na pia baadhi ya madola ya Kiarabu hasa Saudi Arabia.

3586296

captcha