IQNA

Hapa si Syria au Iraq, ni Awamiyah, mji unaohujumiwa kijeshi Saudia+PICHA

12:56 - July 10, 2017
Habari ID: 3471060
TEHRAN (IQNA)-Kwa muda wa takribani miezi miwili mtaa wa al Mosara katika mji wa Awamiyah nchini Saudi Arabia umekuwa chini ya mzingiro wa wanajeshi ambao wametekeleza uharibifu mkubwa na kuwaua raia kadhaa.

Tokea Mei 10 wanajeshi wa Saudi Arabia walivamia mtaa wa Al Mosara mjini Awamiyah katika wilaya ya Qatif mkoa mashariki mwa nchi hiyo ambapo tokea wakati huo wamewaua watu kadhaa na kuteteteza moto misikiti, nyumba za raia na shule katika mtaa huo. Aghalabu ya wakaazi wa eneo la Mashariki mwa Saudia ni Waislamu wa madhehebu ya Shia na wanakandamizwa na utawala wa ufalme wa Kiwahabbi wa Saudia.

Picha zilizoenea katika mitandao ya kijamii hivi karibuni zinaonyesha uharibifu mkubwa uliotekelezwa na wanajeshi katili wa Saudia ambapo kwa mtazamo wa awali utadhani ni picha za maeneo ya kivita ya Syria, Iraq, au Libya. Waandishi habari wamepigwa marufuku kufika eneo hilo na hivyo inakuwa vigumu kwa ulimwengu kufahamu kiwango cha ukatili, uharibifu na jinai dhidi ya binadamu zinazotekeleza na Saudi dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia.

Watawala wa Saudia wanadai wanataka kufanya ukarabati katika mtaa wa kihistoria wa al-Mosara ambako ndiko alikozaliwa Sheikh Nimri Baqir an-Nimr, mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu aliyeuawa kwa kukatwa kichwa na utawala huo mwaka jana.

Wataalamu wa masuala ya turathi katika Umoja wa Mataifa wameutaka utawala wa Saudia usitishe mpango wake wa kuubomoa mtaa huo wakisema ni wa kale na ni turathi ya utamaduni na ustaarabu wa eneo hilo. Hatahivyo watawala wenye kiburi wa Saudia wamepuuza kabisa agizo hilo la Umoja wa Mataifa na wanaendeleza na uharibifu wao.

Raia kadhaa Waislamu wa madhehebu ya Shia wameuawa katika mtaa huo tokea mwezi Mei ambapo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kulishuhudiwa kilele cha jinai za Saudia wakati msomi maarufu wa Qur’ani Tukufu Shahidi Amin al Hani alipIgwa risasi na kuuawa usiku wakati akiwa ametoka katika darsa ya kufundisha Qur’ani.

Kwa upande wa kiuchumi, maeneo hayo ya mashariki mwa Saudia yana umuhimu mkubwa mno kwa utawala wa Aal Saud kwa sababu akiba kubwa ya utajiri wa mafuta, ambayo yanadhamini asilimia 90 ya pato la nchi hiyo inapatikana katika maeneo hayo.

Muundo wa idadi ya watu na utajiri mkubwa wa mafuta ni sababu mbili kuu zinazoufanya utawala wa Aal Saud ushughulishwe mno na pia uwe na ufuatiliaji maalumu kuhusu yanayojiri katika maeneo hayo ya mashariki.

Hata hivyo ufuatiliaji huo unafanyika kwa njia ya uchukuaji hatua kali na maalumu za kiusalama, kwa sababu utawala wa Aal Saud unawahesabu Waislamu wa Kishia kama raia wa daraja la pili; na kutokana na mtazamo wa kimadhehebu ulionao utawala huo pamoja na madhehebu yake ya Uwahabbi kuhusiana na siasa na madaraka, Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaonekana kuwa ni tishio kwa utawala huo wa kifalme wa Aal Saud.

Kwa sababu hiyo, kuwanyongesha, kuwaacha kwenye umasikinina kuwabagua mashia kunafanyika katika utawala wa Aal Saud kwa mbinu na utaratibu maalumu; na hiyo pia ndiyo sababu kuu ya kufanyika maandamano ya upinzani dhidi ya utawala huo wa kiukoo katika maeneo ya mashariki mwa Saudia. Karibu asilimia 20-15 ya raia wa Saudia ni Waislamu wa madhehebu ya Shia.

Picha zilizo hapa chini zinaonyesha uharibifu uliotekeleza na wanajeshi wa utawala wa kiimla wa Aal Saud dhidi ya mtaawa Al Mosara.

Hapa si Syria au Iraq, ni Awamiyah, mji unaohujumiwa kijeshi Saudia+PICHA


Hapa si Syria au Iraq, ni Awamiyah, mji unaohujumiwa kijeshi Saudia+PICHA


Hapa si Syria au Iraq, ni Awamiyah, mji unaohujumiwa kijeshi Saudia+PICHA


Hapa si Syria au Iraq, ni Awamiyah, mji unaohujumiwa kijeshi Saudia+PICHA


Hapa si Syria au Iraq, ni Awamiyah, mji unaohujumiwa kijeshi Saudia+PICHA


Hapa si Syria au Iraq, ni Awamiyah, mji unaohujumiwa kijeshi Saudia+PICHA


Hapa si Syria au Iraq, ni Awamiyah, mji unaohujumiwa kijeshi Saudia+PICHA


Hapa si Syria au Iraq, ni Awamiyah, mji unaohujumiwa kijeshi Saudia+PICHA


3617154

captcha