IQNA

Mashindano ya Qur’ani ya wanawake yafanyika Libya

12:36 - August 20, 2017
Habari ID: 3471131
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya tano ya Qur’ani ya wanawake yanafanyika wiki hii nchini Libya.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo ya Qur’ani Tukufu yalianza Jumamosi katika mji wa Gharyan na yanatazamiwa kuendelea hadi Alhamisi Agosti 24.

Mashindano hayo ya Qur’ani huandaliwa kila mwaka na Jumuiya ya Kiutamaduni ya al-Mahajja al-Bayza. Kwa mujibu wa mkuu wa Jumuiya hiyo, Khayriya Abudina, wanawake 304 wanashiriki katika awamu hii ya tano ya mashindano hayo.

Amesema mashindano hayo yatakuwa na vitengo kadhaa kuanzia kuhifadhi Qur’ani kikamilifu na kuhofadhi juzuu kadhaa.

Maafisa wa utamaduni nchini Libya wanajitahidi kuimarisha harakati za Qur’ani katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini ambayo ilitumbukia katika mapigano ya ndugu kwa ndugu baada ya shirika la kijeshi la nchi za Magharibi NATO kuingilia masuala yake ya ndani na kupelekea kupinduliwa mtawala wa zamani wan chi hiyo Muammar Gaddafi.

3632257

captcha