IQNA

Mjini Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu Yaanza

20:25 - April 27, 2018
Habari ID: 3471485
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Sita ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanachuo Waislamu yameanza katika mji wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yameanza Ijumaa alasiri katika Ukumbi wa Shirika la Utafiti wa Kiislamu katika Taasisi ya Quds Razawi.

Sherehe hizo zimeanza kwa qiraa ya Qur'ani Tukufu ya mshindi wa Mashindano ya Tano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanachuo Waislamu, Bw. Wahid Khazai na kufuatia na hotuba ya Sayyid Hamid Ridha Twaibi, Mkuu wa Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu nchini Iran.Nchi 35 kutoka mabara ya Asia, Afrika, na Ulaya zinawawakilishwa katika mashindano hayo ya wanafunzi Waislamu walio katiak vyuo vikuu ambayo yanatazamiwa kuendelea hadi Aprili 29.Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu Yaanza

Jumuiya ya Harakati za Qur'ani ya Wanaakademia wa Iran inayofungamana na Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR) imekuwa ikiandaa mashindano ya Qur’ani ya wanafunzi Waislamu wa vyuo vikuu baada ya kila miaka miwili tokea mwaka 2006 kwa lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano baina ya wanafunzi Waislamu kote duniani sambamba na kustawisha kiwango cha harakati za Qur’ani katika vyuo vikuu.

3709527

 

captcha