IQNA

Qatar yajenga Msikiti, shule na chuo cha Qur’ani Somalia

22:34 - June 20, 2020
Habari ID: 3472882
TEHRAN (IQNA)- Qatar imefadhili ujenzi wa kituo cha elimu na miradi kadhaa ya maendeleo katika mji wa Kismayo nchini Somalia.

Mradi wa hivi karibuni wa kituo cha Kiislamu kinachojumuisha msikiti, shule na chuo cha kuhifadhi Qur’ani kimefunguliwa katika sherehe iliyohudhuriwa na Naibu Rais wa Jimbo la Jubaland Mohamoud Sayid Adan. Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo Sayid Adan ameishukuru Qatar kwa kuwasiadia wasiojiweza katika jamii kwa kuanzisha miradi yenye thamani.

Naye balozi wa Qatar nchini Somalia Hassan bin Hamza Hashem amesisitiza kuwa nchi yake inasimama pamoja na serikali ya Somalia katika miradi ya maendeleo huku akisisitiza kuhusu umuhimu wa uthabiti Somalia.

Kituo hicho za Kiislamu kinajumuisha shule ya msingi na upili, msikiti, uwanja wa michezo, ukumbu wa mikutano, kituo cha matibabu, madrassah ya kuhifadhi Qur’ani, maduka, na kisima.

3905775

captcha