IQNA

Waislamu Marekani

Jaji wa kwanza wa Marekani Mwislamu mwenye kuvaa Hijabu ataka kuwatetea Waislamu

11:05 - August 29, 2022
Habari ID: 3475697
TEHRAN (IQNA)-Jaji wa kwanza Mwislamu mwenye kuvaa Hijabu katika historia ya Marekani, ambaye alianza kazi yake miezi miwili iliyopita katika hafla ya kiapo kwa Qur'ani Tukufu, anasema kwamba ana nia ya kutetea haki za Waislamu wa Marekani.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya jimbo la Arizona, hakimu wa kike Mwislamu ameteuliwa katika mahakama ya Phoenix.

Leila Ikram aliapishwa kuwa jaji wa muda. Mbali na kuwa Muislamu wa kwanza, Akram pia ndiye jaji wa kwanza katika historia ya Marekani kuvaa hijabu. Pia alikuwa jaji wa kwanza kula kiapo cha yamini kwa Qur'ani Tukufu.  

Akram alisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Arizona cha Sandra D. O'Connor College of Law. Wazazi wake walihamia Marekani kutoka Gaza, Palestina, na kuishi North Carolina.

Akram ameshikilia nyadhifa kadhaa muhimu za kisheria zinazohusiana na mahakama hapo awali. Kabla ya kuteuliwa kuwa jaji wa muda, alifanya kazi kama wakili wa utetezi wa jinai katika Ofisi ya Mwanasheria wa Wilaya ya Maricopa. Leila anataka kuwa sehemu muhimu ya jamii ya Kiislamu inayotafuta haki.

Kuteuliwa kama jaji wa muda ndio mahali pa kuanzia hatua ya kuteuliwa kuwa jaji wa kudumu.

Anasema: "Lengo langu zima la kuwa mwanasheria ni kwamba nataka kutumikia jamii. Kesi za jinai zinajumuisha mzigo mkubwa zaidi wa mahakama. Mahakama ya jinai ni mahali ambapo watu wengi hutatua matatizo yao ya kila siku. Ninahisi nina uwezo wa kusaidia watu haraka na kwa njia ya haki."

Mafanikio ya Ikram kama mwanamke wa Kiislamu ni ya kwanza huko Arizona, lakini hayajawahi kutokea nchini Marekani. Mnamo Januari 2022, Rais wa Marekani Joe Biden aliteua majaji wanane, akiwemo Nusrat Chaudhry, mwanamke wa kwanza Mwislamu kuhudumu kama jaji wa shirikisho.

Mnamo Oktoba 2021, Mwanasheria Mkuu wa Michigan, Fadavi Hammoud, aliweka historia kama mwanamke wa kwanza Mwislamu wa Kiarabu na Amerika kuhudumu katika Mahakama Kuu ya Marekani.

4081550

captcha