IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Nakala Adimu ya msahafu yaonyeshwa kwenye maonyesho ya Riyadh

19:28 - December 19, 2022
Habari ID: 3476272
TEHRAN (IQNA) – Maktaba ya Umma ya Mfalme Abdulaziz huko Riyadh, Saudi Arabia, imeandaa maonyesho ya nakala adimu za Qur'ani Tukufu.

Maonyesho hayo yalifanyika Jumapili, Desemba 18, ambayo yaliadhimisha Siku ya Umoja wa Mataifa ya Lugha ya Kiarabu.

Jumla ya Qur'ani Tukufu 267, nyingi kati ya hizo ni za karne ya 10 hadi 13 Hijria, zilionyeshwa kwenye maonyesho hayo.

Katika hafla hii, maktaba pia iliandaa maonyesho ya maandishi ya Kiarabu yaliyo na kazi katika nyanja tofauti, kama vile lugha ya Kiarabu na fasihi na ensaiklopidia za Kiarabu.

Kulikuwa pia na kazi za kaligrafia pamoja na zaidi ya vitabu 200 kuhusu maandishi ya Kiarabu na uzuri wa maandishi ya Kiarabu na sanaa zinazohusiana.

Siku ya Lugha ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa huadhimishwa kila mwaka mnamo Desemba 18.

Tukio hilo lilianzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mwaka 2010 likitaka "kusherehekea wingi wa lugha na tofauti za kitamaduni pamoja na kukuza matumizi sawa ya lugha zake zote sita za kazi rasmi katika shirika zima".

Tarehe 18 Desemba ilichaguliwa kuwa tarehe ya lugha ya Kiarabu kwani ni siku ya mwaka 1973 ambapo Baraza Kuu liliidhinisha Kiarabu kuwa lugha rasmi ya Umoja wa Mataifa.

Rare Copies of Quran Put on Display at Riyadh Expo

Rare Copies of Quran Put on Display at Riyadh Expo

3481735

captcha