IQNA

Teknolojia

Kongamano la Teknolojia ya Qur'ani Tukufu kufanyika Saudi Arabia

21:20 - February 07, 2024
Habari ID: 3478316
IQNA - Kongamano la teknolojia ya Qur'ani Tukufu limepangwa kufunguliwa katika mji mkuu wa Saudia wa Riyadh wikendi hii. Itahudhuriwa na kundi la wataalam, wasomi na weledi wa teknolojia.

Washiriki watafanya mijadala ya kitaalamu juu ya matumizi ya teknolojia mpya katika kuhudumia Qur'ani Tukufu, tovuti ya Ash-Sharq iliripoti.
Watabadilishana mawazo kuhusu utumizi wa teknolojia mpya ili kuwezesha kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu. 
Wataalamu watakaoshiriki katika kongamano hilo pia watapitia uzoefu wenye mafanikio katika uwanja wa nakala za kidijitali za Qur'ani Tukufu.
Teknolojia ya Blockchain, akili ya memba au AI, na Intaneti ya Vitu ni kati ya nyanja ambazo zitajadiliwa kwenye hafla hiyo.
Hati kadhaa za maelewano (MoUs) pia zinatarajiwa kusainiwa wakati wa kongamano la ushirikiano katika kuendeleza misingi ya kutumia teknolojia mpya katika nyanja za Qur'ani.
Wiki iliyopita, kongamano la kimataifa liliandaliwa nchini Saudi Arabia kujadili changamoto zinazokabili apu za Qur'ani.
Ilihudhuriwa na zaidi ya watengenezaji programu 1,800 kutoka nchi 42.
 
4198439

captcha