IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Iran

Binti wa Ghana aliyeshinda Mashindano ya Qur'ani ya Iran asisitiza kujifunza tafsiri

12:03 - February 23, 2023
Habari ID: 3476613
TEHRAN (IQNA) – Binti hafidh wa Qur’ani Tukufu kutoka Ghana amesisitiza haja ya wenye kuhifadhi Qur'ani Tukufu pia kujitahidi kujifunza tafsiri yake.

Bi. Amina Ibrahim, ambaye alishinda tuzo ya juu katika kitengo cha kuhifadhi (sehemu ya wanawake) ya Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran yam waka huu, amezungumza na mwandishi wa Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) na kusema kuwa kwa kujifunza tafsiri ya Qur'ani, wenye kuhifadhi wanaweza kujifunza zaidi kuhusu mafundisho ya Kitabu hicho Kitukufu ambacho kimeteremshwa kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu.

Aidha aliipongeza Iran kwa kuandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani, akisema matukio kama hayo yanasaidia kuwavutia vijana zaidi kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Alisema mashindano hayo yametoa fursa kwa wanaharakati wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi mbalimbali kujifunza kufahamiana.

Amina Ibrahim pia ameeleza matumaini yake kuwa uhusiano kati ya taasisi za Qur'ani za nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utaimarishwa.

Alipoulizwa kuhusu safari yake ya Qur'ani, binti huyu  mwenye umri wa miaka 18 alisema alianza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa moyo akiwa na umri wa miaka 4 kwa msaada wa familia yake.

Anasema alifanikiwa kuhifadhi Qu'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 14, akibainisha kwamba kaka yake na dada yake pia ni wamehifadhi Qur'ani Tukufu/

Hapo awali Amina aliwahi kushiriki katika Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai mwaka wa 2022 lakini hakuwa miongoni mwa washindi.

Naye Layla Afara kutoka Lebanon, ambaye alihudhuria kategoria ya Tarteel katika sehemu ya wanawake ya mashindano ya Iran, pia alizungumza na IQNA kuhusu mashindano hayo, na kusema kushiriki kwake kumemuwezesha kufahamiana nawanaharakati wa Qur'ani kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Ghanaian Memorizer Underlines Learning Quran Interpretation

Alisema alijifunza Quran na Tarteel katika taasisi kubwa ya Qur'ani nchini mwake. Aliwataja Belqays Harb Jafar na Hajj Adel Mahmoud Khaili kama walimu wake wa Qur'ani Tukufu.

Layla alibainisha kuwa alishika nafasi ya pili katika mashindano ya kitaifa ya Qur'ani nchini Lebanon mwaka jana na ni ushiriki wake wa kwanza katika tukio la kimataifa la Qur'ani.

Alimaliza wa pili katika kitengo cha Tarteel cha shindano hilo.

Wakati huo huo, Nasrin Khaledi kutoka Algeria, ambaye alishika nafasi ya tatu katika kategoria ya kuhifadhi, aliiambia IQNA kwamba alijifunza Qur'ani tangu akiwa mdogo na aliweza kuhifadhi Kitabu hicho kizima kwa msaada wa familia yake.

Ghanaian Memorizer Underlines Learning Quran Interpretation

Alisema ilikuwa ni uzoefu wake wa kwanza kama mshiriki katika hafla ya kimataifa ya Qur'ani, akibainisha kwamba aliwahi kushinda cheo cha juu katika shindano la kitaifa la kuhifadhi Qur'ani nchini Algeria.

Nasrin alibainisha kuwa amesikiliza kisomo cha Kurani kutoka kwa makari wakubwa wa Misri kama Sheikh al-Minshawi na Sheikh al-Husari ili kuhifadhi Qur'ani na kujifunza kusoma.

Pia alisifu kiwango cha mashindano ya Qur'ani ya Iran, kiwango chake kizuri cha mpangilio na ukarimu wa Wairani.

Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran yalihitimishwa kwa hafla ya Jumatano jioni, ambapo washindi wa kategoria tofauti walitajwa na kutunukiwa.

Toleo hili la tukio la kimataifa la Qur'ani lilifanyika katika hatua mbili, huku duru ya kwanza iliyofanyika kwa intaneti miezi kadhaa iliyopita ikiwa imehudhuriwa na wagombea 150 kutoka nchi 80.

Kutoka miongoni mwao, makari 52 na wahifadhi kutoka nchi 33 walifika kwenye fainali, iliyoanza mjini Tehran siku ya Jumamosi.

4123894

captcha