IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Iran

Washindi wa Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran watangazwa, Mkenya ni wa pili

21:01 - February 22, 2023
Habari ID: 3476605
TEHRAN (IQNA)- Washindi wa Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo fainali yake imefanyika wiki hii kwa kuhudhuriwa na washiriki 52 kutoka nchi 33, wametangazwa ambapo mwakilishi wa Kenya ameshika nafasi ya pili katika kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa ripota wa IQNA, washindi wa mashindano hayo wametangazwa leo na kutunukiwa zawadi katika shehrehe ambayo imehudhuriwa na Sayyed Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Washindi wa mashindano hayo ni kama ifuatavyo.

Sehemu ya wanawake

Usomaji Tartil

Fahima Asgharzadeh kutoka Iran, nafasi ya kwanza

Leila Afare kutoka Lebanon, nafasi ya pili

Amina Shirzad kutoka Afghanistan alishika nafasi ya tatu

Kuhifadhi

Amina Ibrahim kutoka Ghana, nafasi ya kwanza

Hajar Mehralian kutoka Iran, nafasi ya pili

Nasreen Khalidi kutoka Algeria, nafasi ya tatu

Sehemu ya wanaume

Usomaji wa Tartil

Mohammad Javad Javari kutoka Iran alishika nafasi ya kwanza

Mohammadyar kutoka Kyrgyzstan alishika nafasi ya pili

Ismail Hamdan kutoka Lebanon, nafasi ya tatu

Usomaji wa Tahqiq

Amirhossein Rahmati kutoka Iran alishika nafasi ya kwanza

Sidamir Hashemi kutoka Afghanistan, nafasi ya pili

Abdullah Fekri kutoka Indonesia alishika nafasi ya tatu

Kuhifadhi

Sina Tabakhi kutoka Iran alishika nafasi ya kwanza

Abdul Aleem Abdul Rahim kutoka Kenya, nafasi ya pili

Sheikh Mahmood Hasan kutoka Bangladesh nafasi ya tatu

captcha