IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Mzee Mwislamu ashambuliwa Uingereza akiwa njiani akitokea Msikitini

16:23 - March 31, 2023
Habari ID: 3476790
TEHRAN (IQNA) – Mzee wa miaka 73 alivamiwa na majambazi watatu alipokuwa akielekea nyumbani baada ya kuswali kwenye msikiti mmoja katika mji wa Birmingham nchini Uingereza.

Muumini huyo mwenye umri wa miaka 73 alikuwa akitembea kando ya barabara wakati watatu hao waliposhuka kwenye gari jeusi kwenye Barabara ya York, mtaani King's Heath.

Mshambulizi mmoja amenaswa kwenye kamera akimpiga teke mzee huyo mgongoni kwa nguvu, na kumfanya aanguke.

Genge hilo lilitoroka eneo la tukio mwendo wa saa tano usiku ya Jumatano jioni huku mwathiriwa akipelekwa hospitalini akiwa amevunjika mkono na majeraha usoni.

Polisi wa West Midlands sasa wameanzisha msako wa kuwasaka washambuliaji huku familia ya mwathiriwa pia ikiomba taarifa kwenye mitandao ya kijamii.

Binti yake aliandika kwenye Facebook: ‘Jana saa tano usiku baba yangu alishambuliwa vikali na kundi la majambazi katika barabara ya York Road alipokuwa akirejea nyumbani kutoka msikitini.

‘Walimvamia kwa nyuma na kumwacha amepoteza fahamu kwenye njia ya miguu huku akitoka damu.

‘Yupo hospitalini. Tafadhali muombee na uwe salama na macho.

‘Pia kama kuna mtu ameona chochote au kusikia chochote, tafadhali, tafadhali naomba uwasiliane na polisi ili tuweze kuwakamata hawa waoga.

Kikosi hicho kilisema hakuna ushahidi wa kupendekeza shambulio hilo lilihusishwa na watu wawili kuchomwa moto karibu na misikiti ya Edgbaston, Birmingham, na Ealing, magharibi mwa London.

Washambuliaji hao wanaelezwa kuwa ni wanaume wawili wazungu na mtu mmoja mweusi, wote wakiwa na umri wa kati ya miaka 18 na 30. Wote walikuwa wamevalia suti.

Kiongozi wa Halmashauri ya Jiji la Birmingham Ian Ward alisema: ‘Hili lilikuwa ni shambulio dhidi ya mzee mmoja aliyekuwa akitoka msikitini  na mawazo yetu yapo kwa mwathiriwa na familia yake kwa wakati huu.

‘Madiwani wa kata na timu ya Usalama wa Jamii wanazungumza na familia na Polisi wa Midlands Magharibi na wataendelea kutoa msaada.

‘Maafisa wa halmashauri na madiwani wa eneo hilo pia wamekuwa wakishirikiana na vikundi vya jamii na misikiti  ili kutoa msaada kwa jamii kubwa.

'Tunaomba kila mtu afanye kazi na polisi na kuepuka uvumi wowote katika hatua hii - na tungependa kushukuru jumuiya ya eneo hilo kwa nia yao ya kushiriki habari juu ya tukio hili.'

3482998

captcha