IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu /28

Juhudi za miaka Saba za kutafsiri Qur'ani Tukufu katika lugha ya Rwanda

20:51 - August 13, 2023
Habari ID: 3477430
TEHRAN (IQNA) – Sheikh Harun, ambaye ni mhubiri wa Kiislamu kutoka Rwanda, alitumia miaka saba kutafsiri Qur'ani Tukufu katika lugha rasmi ya nchi yake.

Rwanda ni nchi ya Mashariki na Kati mwa Afrika. Rwanda ikiwa na digrii chache kusini mwa Ikweta, inapakana na Uganda, Tanzania, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kinyarwanda kinachojulikana rasmi kama Ikinyarwanda, ni lugha ya Kibantu na lugha ya taifa ya Rwanda.

Sheikh Harun alizaliwa mwaka 1969 katika mkoa wa Gitamada nchini Rwanda. Alianza kuhudhuria masomo ya usomaji wa Qur'ani akiwa na umri wa miaka minne na miaka miwili baadaye alijiunga na Shule ya Nizamiya katika mji aliozaliwa.

Mnamo 1979, kituo cha Kiislamu kilianzishwa kwa pamoja katika mji mkuu wa Rwanda wa Kigali na Libya na Umoja wa Falme za Kiarabu. Harun aliondoka katika Shule ya Nizamiya kuendelea na masomo yake katika kituo cha Kiislamu, ambacho walimu wake walikuwa kutoka Sudan na Libya na ambako masomo yalitolewa kwa Kifaransa.

Sheikh Harun alihifadhi nusu ya Qur'ani Tukufu katika kituo hicho na kuanza kuhubiri Uislamu.

Mnamo 1997, alienda Kenya kuhudhuria shule ya Kiislamu huko. Alikutana na mwanachuoni maarufu wa madhehebu ya Shia Sheikh Abdullah Nassir hapo na akapewa jukumu na chuo chake kuzungumza naye kuhusu sababu iliyo mpelekea kufuata Uislamu kwa mujibu wa madhehebu ya Shia. Katika mazungumzo haya,  Sheikh Harun alipendezwa na Ushia na hivyo nayo akaamua kufuata madhehebu ya Shia.

Baada ya kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda, Sheikh Harun alikimbilia Tanzania na huko alikutana na mwanazuoni wa Kiisalmu kutoka Iran aitwaye Sheikh Hassan Mohajer, ambaye kwa msaada wake aliendelea na kazi yake ya kuhubiri.

Kwa kuzingatia kuenea kwa Uislamu nchini Rwanda na kutokana na kkuwa Wnayarwanda wengi walikuwa wanavutiwa na Uislamu,  kulikuwa na uhitaji wa kutafsiri vitabu vya Kiislamu katika lugha ya Kinyarwanda. Kwa hiyo, Sheikh Harun alianza kutafsiri vitabu hivyo.

Alifasiri kubwa ya vitabu vya Kiislamu katika lugha ya Kinyarwanda ikiwa ni pamoja "Historia ya Muhammad (SAW) na Makhalifa", "Shia na Quran", "Shia na Hadith", Shia na Sahaba (maswahaba wa Mtume)", na "Asl Ash-Shia".

Mnamo mwaka wa 2010, alipokuwa akisoma nchini Iran, Sheikh Harun alianza kutafsiri Qur'ani Tukufu katika lugha ya Rwanda na ilimchukua miaka 7 kukamilisha tafsiri hiyo.

Habari zinazohusiana
captcha