IQNA

Maonyesho ya Qur'ani Tukufu

Tarehe ya Kuanza Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

16:08 - December 27, 2023
Habari ID: 3478099
IQNA - Maonesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yatazinduliwa siku ya 5 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ripoti zisizo rasmi zilidokeza jana.

Duru zimebaini kuwa maonyesho hayo yataendelea hadi siku ya 18 ya mwezi huo mtukufu.

Akizungumza na IQNA, Mohammad Mehdi Aziz-Zadeh, afisa wa Idara ya Qur'ani na Etrat ya Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu ya Iran, hakuthibitisha ripoti hizo. Alisema tarehe za ufunguzi na kufungwa kwa maonyesho hayo zimewekwa lakini zinaweza kubadilika. Ukumbi wa Imam Khomeini (RA) Mosalla (ukumbi wa Swala), ambao utakuwa uwanja wa maonyesho yajayo, pia huandaa Sala ya Ijumaa na, kwa hiyo, kubainisha tarehe kamili ya maonyesho hayo kunahitaji uratibu na Makao Makuu ya Kusimamisha Sala ya Ijumaa aliyobainisha.

Baraza la utungaji sera la maonyesho hayo linafanya mazungumzo na makao makuu kuhusu suala hili, aliongeza.

Maonesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza dhana za Qur'ani Tukufu na kuendeleza shughuli za kitabu hicho Kitakatifu.

Inaonyesha mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani Tukufu nchini humo na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

Mapema mwezi huu, Waziri wa Utamaduni wa Iran Mohammad Mehdi Esmaeili, alitoa wito wa kutekelezwa mawazo mapya ili kuimarisha tukio la kimataifa la Qur'ani Tukufu.

Aidha amebainisha kuwa Ramadhani inayokuja inasadifiana na sikukuu ya Nowruz (Mwaka Mpya wa Iran) nchini Iran, ambayo inatoa fursa kwa watu kunufaika zaidi na shughuli za maonyesho hayo.

4189589

Habari zinazohusiana
captcha