IQNA

Diplomasia ya Qur’ani

Afrika ni kituo cha kwanza cha Diplomasia ya Qur’ani

16:28 - March 23, 2024
Habari ID: 3478561
IQNA - Kongamano lililopewa jina la "Hadhi ya Qur'ani Tukufu katika Afrika ya Sasa" lilifanyika katika Maonyesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu Ijumaa usiku.

Likiwa limeandaliwa na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA)- Kongamano lililopewa jina la "Hadhi ya Qur'ani Tukufu katika Afrika ya Kisasa" lilifanyika Ijumaa usiku na kuhudhuriwa shakhsia wa Qur'ani kutoka Tunisia na Algeria.

Mzungumzaji katika kikao hicho, Seyed Hassan Esmati katika hotuba yake aliashiria uwepo wa wasomaji Qur'ani katika kasri ya  mfalme wa Abyssinia (Ethiopia ya leo) katika miaka ya mwanzo baada ya ujio wa Uislamu na kusema kwa hakika bara la Afrika lilikuwani kituo cha kwanza cha diplomasia ya Qur'ani.

Mzungumzaji mwingine alikuwa Omar bin Ali al-Jamani, mwandishi wa kaligrafia ya Qur’ani kutoka Tunisia ambaye alifafanua juu ya historia ya uwepo wa Uislamu katika nchi yake.

Pia amesema sanaa za Qur'ani zina mizizi katika historia ya Tunisia na Andalusia.

Al-Jamani aliangazia zaidi jukumu muhimu la Chuo Kikuu cha Ez-Zitouna katika shughuli za Qur'ani Tunisia.

Kwingineko katika maelezo yake, alisema Mus’haf nyingi zimenakiliwa nchini Tunisia, ukiwemo Mus’haf Tijani Mohammadi  na Mus’haf al-Miratiya na akabainisha kwamba yeye mwenyewe, ameandika Mush’af amba u­­tachapishwa katika siku za usoni.

Msomi wa chuo kikuu na mwanaharakati wa Qur'ani Armouli Bilal kutoka Algeria pia alihutubia kongamano hilo.

Aliangazia mapenzi ya watu wa Algeria kwa Qur’ani, ambayo yanadhihirika katika idadi kubwa ya Maktab (shule za jadi za Qur'ani ambazo Afrika Mashariki hujulikana kama Madrassah au Duksi).

Alisema makumi ya maelfu ya Maktab zinaendeleza shughuli za masomo ya Qur’ani nchini Algeria leo.

Maonesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yalizinduliwa Jumatano Machi 20 katika ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini (RA).

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza ufahamu Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani.

Huonyesha mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani nchini Iran na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

 

3487695

Habari zinazohusiana
captcha