IQNA

Mabasi ya London yana mabango ya 'Subhan Allah' katika Kampeni ya Mwezi wa Ramadhani

19:22 - May 10, 2016
Habari ID: 3470304
Shirika moja la kutoa misaada nchini Uingereza limeanzisha kampeni ya matangazo yenye mabango ya 'Subhan Allah' kwa ajili ya kushajiisha watu watoe misaada katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Shirika la kimataifa la kutoa misaada lijulikanalo kama Islamic Relief limelipia mabango katika mabasi hayo.

Gazeti la Independent limeripoti kuwa baadhi ya vyombo vya habari vimekosoa kampeni hiyo kwa madai kuwa kuweka mabango kama hyo katika mabasi ya umma kunawaudhu wasiokuwa Waislamu. Wanaopinga mabango hayo wanasema hivi karibuni sinema za Uingereza zilikataa kutangaza tangazo la kidini la Kanisa la England.

Hatahivyo msemaji wa Islamic Relief Martin Cottingham amesema si sahihi kulinganisha maudhui hizo mbili. Amesema tangazo la Islamic Relief ni sawa na kampeni za ukusanyaji pesa za mashirika ya misaada ya mashirika ya Kikristo kama vile Christian Aid au Tearfund ambayo huweka matnagao pasina kuwepo utata. Amesema Islamic Relief si shirika la kuhubiri bali ni shirika ambalo hukusanya misaada ambayo huwafikia watu wa dini zote. Ameongeza kuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Waislamu hukusanya misaada kwa ajili ya wasiojiweza katika jamii. Kamepni hiyo ya Subhan Allah, inatazamiwa kuzinduliwa katika miji mingine ya Uingereza Ijumaa hii. Msemaji huyo amebaini kuwa misaada inayokusanyw akupitia tangazo hilo itasaidia miradi ya shirika hilo huko Bangladesh, Kenya, Syria na Ukanda wa Ghaza.

Waislamu nchini Uingereza hutoa takribani Pauni milioni 100 kila mwaka wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani huku Shirika la Islamic Relief kila mwaka likikusanya katraibani Pauni milioni 20 katika kampeni ya misaada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

3459766

captcha