IQNA

Misikiti London yapokea vitisho kutoka magaidi wa mrengo wa kulia

18:09 - July 09, 2016
Habari ID: 3470442
Misikiti kadhaa mjini London imepokea vitio vya kigaidi kutoka kwa makundi yanayoamnikiwa kuwa ya wabauguzi wa mrengo wa kulia huku vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu vikiongezeka nchini humo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, misikiti kadhaa London imepokea vifurushi vyeney poda nyeupe huku kukiwa na maandishi ya kibaguzi dhidi ya Waislamu jambo ambalo limepelekea idara ya kupambana na ugaidi nchini humo kuanzisha uchunguzi.

Vifurishi hivyo vilitumwa Alhamisi katika misikiti mitatu ya Masjid Ayesha Tottenham, Masjid Noor ul Islam Leyton na Masjid Finsbury Park yote ya mjini London.

Kifurushi kimoja pia kilitumwa kwa Lord Nazir Ahmed ambaye ni mjumbe katika Bunge la Malodi la Uingereza ambaye pia alipokea matusi katika kufurushi chake.

Maafisa wa misikiti hiyo walilazimika kuvalia mavazi maalumu wakati uchunguzi ukifanyika ambapo misikiti hiyo pia ilifungwa kwa muda. Idara ya Upelelezi ya Scotland Yard imesema inachunguza vitisho dhidi ya misikiti na Waislamu.

Tokea Waingereza wapige kura ya kujuiondoa Umoja wa Ulaya maarufu kama Brexit Juni 23, Waislamu Uingereza wanakabiliana na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu ambapo wanawake wanaovaa Hijabu ndio wanaoathiriwa vibaya zaidi.

Baraza la Waislamu Uingereza limesema kulijiri hujuma 100 za chuki dhidi ya Waislamu katika wikendi ya kwanza kufuatia kura hiyo ya maoni. Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Uingereza Shuja Shafi ametahadharisha kuhusu viterndo vya kushtua vya chuki dhidi ya Waislamu na jamii za waliowachache nchini humo na ameitaja hali hiyo kuwa mgogoro wa kisasa unaohatarisha Amani ya kijamii.

Ugaidi wa mrengo wa kulia unaongezeka kwa kasi na unachochewa na itikadi za wazungu wa mrengo wa kulia wenye misimamo mikali ambao wanapinga watu wasiokuwa wazungu na hasa Waislamu. Ugaidi wa aina hii unapuuzwa na jamii ya kimataifa huku Waislamu wakiendelea kuwa waathirika wakuu.

3460333

Kishikizo: london ugaidi waislamu
captcha