IQNA

Mwanamke Mwislamu avuliwa Hijabu barabarani London

15:57 - October 10, 2016
Habari ID: 3470607
Mwanamke Mwislamu amehujumiwa na kuvuliwa Hijabu katika hujuma ya kibaguzi iliyojiri mjini London.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mwanamke huyo aliye na umri wa miaka 20, alihujumiwa Jumatano iliyopita alipokuwa akitimebea katika eneo la Haringey, London Kaskazini, akiwa na rafiki yake majira ya saa moja na nusu jioni.

Mwanamke huyo anasema alipokuwa akivuka barabara karibu na Chuo cha Haringey na Einfiled, aliandamwa na wanaume wawili ambapo mmoja mmoja wao alimgonga na kuvua hijabu aliyokuwa amevaa kabla ya wawili hao kutoroka.

Mwanamke huyo Mwislamu ameripoti tukio hilo katika Idara ya Polisi London na kusema alipata mshtuko mkubwa kutokana na tukio hilo. Imedokezwa kuwa waliotekeleza hujuma hiyo ni Wazungu wenye misimamo ya kibaguzi na chuki dhidi ya Uislamu.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko kubwa la vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya na kuwafanya Waislamu kuingiwa na wasiwasi zaidi siku baada ya siku. Hii ni katika hali ambayo, serikali za nchi za Ulaya badala ya kulishughulikia tatizo la chuki na hofu dhidi ya Uislamu (Islamophobia) na kulipatia ufumbuzi, wamebaki kimya; na wanapozungumza wanatumia visingizio vya hujuma za kigaidi, ambazo Waislamu wanalaani kila siku, kuhalalisha uafiriti unaofanywa na raia wao dhidi ya jamii ya Waislamu.

3461132

captcha