IQNA

Kiongozi wa Hizbullah

Utawala haramu wa Isael ni tishio kuu kwa usalama Mashariki ya Kati

12:26 - May 26, 2016
Habari ID: 3470337
Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ndio tishio kuu kwa usalama na amani Mashariki ya Kati

Sayyid Hassan Nasrullah aliyasema hayo Jumatano mjini Beirut kwa mnasaba wa Siku ya Mapambano na Ukombozi, ambapo wananchi wa Lebanon wanaadhimisha miaka 16 tangu jeshi la utawala ghasibu wa Israel likimbie kwa madhila kutoka kusini mwa Lebanon na kusisitiza kuwa, njia pekee ya kuuzuia utawala huo haramu kutanua wigo na kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wake ni muqawama na kusimama kidete.

Sayyid Nasrullah amesema kuadhimishwa na kuenziwa siku hii kunaonyesha kuwa harakati ya muqawama inajivunia na kuona fahari kwa mafanikio iliyopata dhidi ya utawala haramu wa Israel.

Amesema: "Ushindi huu ni sehemu ya utamaduni na historia ya Lebanon, ili kuvifunza vizazi vijavyo namna ya kusimama kidete kupinga udhalimu. Harakati hii imeutoa ushindi wa siku hii kwa ajili ya Wapalestina na dunia nzima kwa ujumla."

Itakumbukwa kuwa, mwezi Mei mwaka 2000, askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel walikimbia kwa madhila kusini mwa Lebanon, baada ya kufurushwa na wanamapambano wa Hizbullah.

3501231

captcha